Toka mzee wetu azaliwe na kubahatika kumpata mke wa kwanza wa kumtunza Februari 5, 1977 na kuwa mama wa Watanzania wote bara na visiwani kwa miaka mingi, hatimaye mwaka 1992, mzee kwa kushirikiana na mke mkubwa, aliweka wazi wazo lake la kuwa na wake wengi.
Wakaibuka wengi kwa namna ambayo haikutarajiwa NCCR MAGEUZI, CUF, CHADEMA, ACT WAZALENDO, DP, na wengine wengi huku kila mmoja akitamani kuwa katika mstari wa mbele wa kumlea mzee wetu Tanzania.
Wamefanya hivyo mara nyingi lakini nguvu ya mke mkubwa imekuwa haiwapi fursa ya kufurukuta na kufikia malengo kusudiwa katika malezi ya Mzee Tanzania.
Ni kipi kinachomfanya Bibi mkubwa kutotaka kuwapa wake wenza nafasi ya kumhudumia mzee?
Je, ni kweli ushawishi wa Bibi mkubwa kwa watoto wa Mzee Tanzania watokanao wake zake mbalimbali ni mkubwa kiasi cha kukubali yeye ndie amlee mzee kwa wakati wote?
Je, watoto wengi aliowazaa Bi mkubwa hawaoni kwamba nguvu zimemuishia na Mzee anahitaji kuendelea kupata huduma kutoka kwa wake zake wadogo?
Je, sisi watoto wa Mzee maoni yetu ni yapi tunapokaribia miaka mingine ya kuamua ni nani ashikilie malezi ya mzee?
Bi mkubwa atakuwa tayari kuwapa wake wenza majukumu ya kumlea mzee ambae wana historia ndefu ya maisha?