Sauti ya Umma
Member
- Aug 26, 2010
- 39
- 21
HABARI,
Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC mapema tarehe 25 Agosti 2020 ilimteua Ndugu MWAKASAKA BOAZ DONARD kuwa mgombea ubunge Jimbo la Ubungo kupitia Chama Cha Sauti ya Umma (SAU). Mwakasaka ni mtaalamu wa masuala ya Uchumi na Maendeleo ya kijamii ameahidi kutokomeza yote yaliyoshindikana katika Jimbo la Ubungo na amesema atatumia uwezo wake wa kuelewa bila kufikiri kutatua changamoto za Jimbo la Ubungo.
Mwakasaka amepanga kufanya Kampeni za kihistoria ambazo hazijawahi kutokea tangu taifa hili lianzishwe na kwamba ana ujumbe maalumu kwa wananchi wa Ubungo na taifa kwa ujumlautaoleta Uamsho wa maendeleo kwa mtu mmoja mmoja, uamsho ambao haujawahi kutokea tangu kuwekwa misingi ya Ulimwengu huu.
Bwana Mwakasaka anawaomba wananchi wa Jimbo la Ubungo na nje ya Jimbo hilo wajitokeze kwa wingi sana kushiriki katika kampeni za kiumbe huyu wa pekee na ambaye ni tunu ya pekee kwa taifa la Tanzania.
Lakini zaidi sana anawaomba wagombea wenzake wote wajitokeze kusikiliza hotuba zake kwani zitawasaidia kupata ulewa wa masuala yenye tija kwa kizazi hiki na vizazi vijavyo.
Bwana Mwakasaka anatarajia kuanza kampeni zake mapema mwezi septemba 2020 na atafanya kampeni zake kwa miguu na hatatumia vikundi vya sanaa na ngoma kwani muda wa kutosha unahitajika kwa ajili ya kufikisha ujumbe kwa wananchi ujumbe utakaowasha moto wa maendeleo ndani ya jimbo la Ubungo na taifa kwa ujumla.
HII SI YA KUKOSA