Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Sambamba na hilo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mzee wa miaka 80 mkazi wa Kijiji cha Madundasi Wilaya ya Mbarali Mkoa wa Mbeya aitwaye PASCAL MWANGO kwa tuhuma za kupatikana na bunduki aina ya Gobole bila kuwa na kibali cha umiliki halali.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema Mtuhumiwa alikamatwa Oktoba 20, 2023 huko Masenjele ndani ya hifadhi ya taifa ya Ruaha wakati Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Askari wa Jeshi la Uhifadhi - TANAPA likiwa katika misako na doria dhidi ya wawindaji haramu na majangiri wanaofanya uhalifu ndani ya hifadhi ya Taifa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga
Katika upekuzi alikutwa na bunduki moja [gobole], risasi [golori] 35, unga wa baruti ukiwa kwenye mfuko wa plastiki, kisu 01, kiberiti 01 na fataki mbili za kulipulia bila kibali cha umiliki halali wa vitu hivyo. Mtuhumiwa amekuwa akifanya uhalifu kwa kuwinda na kuua Wanyama pori ndani ya hifadhi ya Taifa ya Ruaha.
Jeshi la Polisi lipo katika kampeni ya msamaha wa usalimishaji silaha haramu kwa hiari iliyoanza Septemba mosi na inatarajiwa kumalizika Oktoba 31, 2023.
Hivyo ni wito wa Jeshi la Polisi kwa wananchi wote wanaomiliki silaha kinyume cha sheria kusalimisha kwa hiari katika vituo vya Polisi, ofisi za serikali za mitaa na ofisi za watendaji wa Kata. Muda wa kusalimisha silaha ni kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi 10:00 jioni. “Hujachelewa, salimisha silaha sasa katika kipindi cha msamaha”
Pia katika muendelezo wa Misako, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa sita kwa tuhuma za wizi wa mali zinazosafirishwa kwa magari. Watuhumiwa waliokamatwa ni:-
Wamekutwa na Bajaji moja MC 689 CMX aina ya TVS Kings ambayo hutumika kubeba mizigo inayoibiwa, Spika moja na mifuko sita ya Soya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema Mtuhumiwa alikamatwa Oktoba 20, 2023 huko Masenjele ndani ya hifadhi ya taifa ya Ruaha wakati Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Askari wa Jeshi la Uhifadhi - TANAPA likiwa katika misako na doria dhidi ya wawindaji haramu na majangiri wanaofanya uhalifu ndani ya hifadhi ya Taifa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga
Jeshi la Polisi lipo katika kampeni ya msamaha wa usalimishaji silaha haramu kwa hiari iliyoanza Septemba mosi na inatarajiwa kumalizika Oktoba 31, 2023.
Hivyo ni wito wa Jeshi la Polisi kwa wananchi wote wanaomiliki silaha kinyume cha sheria kusalimisha kwa hiari katika vituo vya Polisi, ofisi za serikali za mitaa na ofisi za watendaji wa Kata. Muda wa kusalimisha silaha ni kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi 10:00 jioni. “Hujachelewa, salimisha silaha sasa katika kipindi cha msamaha”
Pia katika muendelezo wa Misako, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa sita kwa tuhuma za wizi wa mali zinazosafirishwa kwa magari. Watuhumiwa waliokamatwa ni:-
- MUSA MSWIMA [27] Fundi radio, mkazi wa Mapelele
- KELVIN ENOCK [29] Mkazi wa Tarafani
- EMMANUEL IBRAHIM [29] Dereva bajaji, mkazi wa Mapelele
- MIKIDADI IMANI [28] Mkazi wa Nsalala
- MAJALIWA ANDULILE [38] Mkazi wa Tarafani
- BARAKA MWANSASU [30] Mkazi wa Nzovwe