Mzee wa upako ateswa na MISUKULE!

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,277
Reaction score
8,860
MBALI na Askofu wa Kanisa la Full Gosple Bible Fellowship, Zacharia Kakobe kuteswa na misukule inayodaiwa kufufuliwa na baadhi ya makanisa ya kiroho nchini, Mchungaji wa Kanisa la Maombezi
Akizungumza na Uwazi juzi, Mzee wa Upako alisema suala la misukule linamtesa sana na kwamba anapingana na kufufuliwa kwao na baadhi ya wachungaji wa makanisa mbalimbali wanaojigamba kufufua misukule wakati si kweli na ni utapeli mtupu.
MZEE WA UPAKO ANAFUNGUKA:
“Kuna baadhi ya viongozi wa makanisa ya kiroho (bila kutaja majina) wanadanganya watu kuwa wanatoa misukule, si ukweli kabisa ni uongo. Wanatafuta namna ya kula sadaka za waumini wao kwa kuonekana wanaweza sana mambo ya kiroho,” alisema Mzee wa Upako na kuongeza:
“Hawa wachungaji wanatuchafua sana sisi tunaosimamia Neno la Mungu, wanaharibu Kanisa la Mungu kwa kudanganya waumini wao kwa sababu ya pesa tu. Hebu fikiria kuna wengine wanatoa hadi shilingi 400,000 kwa mtu ili akubali kufanywa msukule feki na baadaye aombewe kanisani tena nimesikia wanatengenezewa hati za kifo kuonesha kuwa kweli watu hao walifariki dunia wakati si kweli, wamwogope Mungu.
“Huo ni usanii ndani ya Kanisa la Mungu. Nasema naumizwa sana na wachungaji wa namna hii, nateseka sana na hili jambo. Ninayo mpaka CD za mahubiri za baadhi ya viongozi wa makanisa wanaodanganya kuwafufua misukule lakini kwa busara siwezi kuwataja ila wanajijua kwa sababu hata dhamira zao zinawashuhudia.”
TURUDI KWA KAKOBE
Akikazia zaidi, Askofu Kakobe alisema, anayedai ana uwezo wa kufufua misukule ni muongo na kwamba atakuwa anaabudu shetani.
“Mwenye uwezo wa kufufua ni Yesu Kristo pekee na alifanya hivyo kwa sababu ya utukufu wa Mungu na si vinginevyo, si binadamu wa kawaida ambaye amepewa upako wa Mungu anadanganya watu kuwa anao uwezo wa kumtoa mtu ambaye alichukuliwa msukule,” alisema Askofu Kakobe huku akisisitiza kwamba mtumishi yeyote wa Mungu anaweza kufanya muujiza huo kwa utukufu wa Mungu lakini si kwa sababu ya kuonesha yeye anaweza.
 
Kwa hiyo yule jamaa wa kanisa la ufufuo na uzima ni muongo? Ngoja waje wafuasi wake watuambie
 
Mh mnapenda usutwa na watumishi wa mungu, nyiw pia misukule tu, mtafufuliwa sio muda
 
Wanasemaje viongozi wa Baraza Pentekoste Tanzania(PCT) kuhusu utata wa "MISUKULE" ?

MSAADA:"Hivi kazi ya PCT ni nini ?!
 
ujinga wa waumini ujanja wa machungaji.....
 
Inasikitisha mch. Kumsema vibaya mch. Mwenzake ingawa najua vita kubwa uwa ni waumini na sio kingine.
 
Watanzania wote ni misikule ya ccm kujiondoa usikuleni ni kujitambua kwa kuikataa.
 
Watanzania wote ni misikule ya ccm kujiondoa usikuleni ni kujitambua kwa kuikataa.

Mkuu,tumia busara,kama wewe ni msukule usituite wengine misukule,kama unajua maana ya msukule basi usingeandika hii sentebsi,hebu kueni makini sana na maneno yenu humu janvini,tusijitamkie maneno ya ajabu wakati sisi badio tunaishi,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…