Mzee wa Upako: Nampenda Diamond kwa sababu ni mnyenyekevu, simpendi Alikiba ni kiburi

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2018
Posts
882
Reaction score
3,337
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo maarufu kwa jina la Mzee wa Upako, amemtaja msanii ambaye anamkubali kati ya Alikiba na Diamond pamoja na kutoa sababu zake

Akiongea na kipindi cha Maisha Mseto cha Times FM, Mzee huyo wa Upako amesema anampenda sana Diamond kwa sababu ni mnyenyekevu lakini Alikiba ni kiburi.

“Mimi nampenda sana Diamond kwa sababu ni mnyenyekevu, Simpendi Alikiba kwa sababu ana kiburi, nadhani kwa sababu amekaa Kariakoo,” amesema Lusekelo.

Mchungaji huyo ameongeza kwa kusema, “Ukipigia simu Diamond anapokea kwa unyenyekevu ila Alikiba anapokea kwa maringo. Ndio maana Diamond amefika mbali.”
 
Mzee wa upako anakuwa kama muuza bucha aliyetaka kumuibia mama kuku wa kilo moja na nusu amuuzie kwa bei ya kilo 2. Cc. Bujibuji
Ila tusiwaseme vibaya masihi wa Bwana.
Mwanamama anaingia katika bucha , muda mfupi kabla ya kufungwa bucha na anamuuliza muuza nyama:
"Una kuku?
Muuza bucha anafungua friji yake na kumtoa kuku mmoja tu aliyebaki hakukua na kuku mwingine zaidi ya huyo kuku.
Akamuweka kwenye mzani kumpima ikaonekana huyo kuku ana kilo moja unusu.
Yule mama akauliza tena
"... je hauna kuku mkubwa zaidi ya huyu tafadhali...?
Ujanja wa kibiashara na tamaa ukamuingia muuza kuku,
Akajifanya kumchukua yule kuku kumrudisha kwenye friji , halafu akajifanya anamtoa kuku mwingine na kumuweka kwenye mzani na kwa ufundi na umahiri mkubwa wa kiujanja ujanja ,alipomuweka yule kuku kwenye mzani akaweka kidole chake kwenye mzani kiudanganyifu , mizani ikasoma kilo mbili
Yule mama akaagiza "nifungie wote wawili, yule uliyemrudisha na huyu wa sasa"
Ni hayo tu kwa sasa...
 
Ndiyo ''mitume'' na ''wachungaji'' wetu wa kisasa. Ama kweli wajinga ndiyo waliwao. Unakuta tapeli kama huyu amefungisha tela wa manyumbu maelfu kadhaa na wanampelekea fedha kanisani!
Akiwemo mwenyekiti wako mtukufu, kiongozi wa malaika aliyemuahidi kumwekea lami mpaka madhabahuni?

Kumbe manyumbu yako ya aina tofauti tofauti...

La mikumi haliwezi kuwa sawa na la Serengeti
 
Kila nikilala nikiota ndoto naota kabisa huyu muuza bucha ni GuDume
 
Ndiyo ''mitume'' na ''wachungaji'' wetu wa kisasa. Ama kweli wajinga ndiyo waliwao. Unakuta tapeli kama huyu amefungisha tela wa manyumbu maelfu kadhaa na wanampelekea fedha kanisani!
Kamtapeli nani? Yeyote aliye tapeliwa na BOB LUSE MZEE wa Upako aje kwangu nimsaidie kusimamia haki yake mpaka ipatikane.
macho_mdiliko, jihadhari na kitu kinaitwa defamation, unaweza kujikuta hatiani iwapo utashindwa kuuthibitisha utapeli wa Lusekelo
 
Akiwemo mwenyekiti wako aliyemuahidi kumwekea lami mpaka madhabahuni?

Kumbe manyumbu yako ya aina tofauti tofauti...

La mikumi haliwezi kuwa sawa na la Serengeti
Hiyo lami ni kwa ajili ya watu wa kibangu sio waumini ws mzee wa upako wanaoitumia mara moja kwa wiki
 
Amefikaje huko kuwazungumzia wasanii...!?

Tupeni hiyo interview hapa.
 
Ndiyo ''mitume'' na ''wachungaji'' wetu wa kisasa. Ama kweli wajinga ndiyo waliwao. Unakuta tapeli kama huyu amefungisha tela wa manyumbu maelfu kadhaa na wanampelekea fedha kanisani!
Umesahau kuwa hata mwenyekiti wa manyumbu ya kijani alienda kanisani kwake kumpelekea sadaka na ahadi ya lami.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…