Mzee wa Upako: Nampenda Diamond kwa sababu ni mnyenyekevu, simpendi Alikiba ni kiburi

Kimbieni kutoka kati ya Babeli, mkatoke katika nchi ya Wakaldayo, mkawe kama mabeberu mbele ya makundi. => YEREMIA 5O:8
 
Watu wangu wamekuwa kondoo waliopotea, wachungaji wao wamewapoteza; wamewapotosha milimani; wamekwenda toka mlima hata kilima, wamesahau mahali pao pa kupumzika. =>YEREMIA 50:6

Mambo ni fire Bujibuji
 
Ni kweli Ali ana kiburi sana sema wachache wanaweza kugundua tabia yake hiyo.
 
tukienda kanisani ni hawahawa wanaotufundisha KUMPENDA KILA MTU HATA AWE ADUI YAKO.... kumbe wenyewe wana chuki za wazi kabisa.


#any way, pengine aliyazungumza haya akiwa amekunywa mvinyo,, maana huyu mchungaji nasikia ni chapombe sana.
 
Angesoma philosophy hangeonyesha chuki dhidi ya mtu hususa yeye ni mchungaji ngazi ya upako. I'm doubting about mzee wa upako
 
Mchungaji anapaswa kuwapenda wote na "kumuombea" yule mwingine ili hicho kibri kiondoke. Wachungaji hawa wa kidigitali hawana maadili hata kidogo
 
Ni kweli Ali ana kiburi sana sema wachache wanaweza kugundua tabia yake hiyo.
Nimesema sana hili,hata hao wanaombeba wanalijua hili ila wanavumilia tu hawana namna,kwakuwa lengo lao ni kumshusha huyo mmoja.

Ali ni kiburi,jeuri,anajiona ni boora,na kama yeye ndio angekuwa na mafanikio kama ya Diamond, Tanzania ingesimama kwa madharau yake.
 
Ni kweli na sisi wakristo Biblia inasema kuwa Mungu huwapinga wenye kiburi.
 
Ni kauli ya hovyo sana kutolewa na mlezi wa kiroho, huu ni upofu wa hali ya juu.
Kazi kuu ya mchungaji ni kitafuta kondoo aliyepotea.
Mfano; mlevi, mzinzi, mwenye kiburi nk.
Leo unatamka hadhari humpendi mwenye kiburi, je! Waweza kumhubiria injili aokoke?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…