Nimekuwa nikimsikia huyu mchungaji Lusekelo maarufu kama mzee wa upako akieleza baadhi ya kweli zinazoongewa kwa mihemko na Wakristo wanafiki wanaokuwa mahakimu kuhukumu wengine wanaodhani ni wadhambi kwa jinsi wanavyolisoma na kulielewa neno.
Nakubaliana naye kuwa kunywa pombe sio dhambi lakini pombe haiwafai wafalme. Katika dunia hii ni eidha uchague kuwa mfalme au maskini. Maana imeandikwa mpe maskini pombe ili asahau shida zake.
Pili nakubaliana naye kuwa ukikuta mwanamke sio bikra,ujue umeoa mke wa mtu. Mke wa ujana wako ni yule uliyemkuta bikra.Ndoa ni tendo la ndoa na wala sio zile mbwembwe za kanisani.Hizo ni taratibu za watu binafsi waliozitunga kwa msaada wa ibilisi ili ziwe mtego kwa wana wa Mungu wahukumiwe dhamiri zao wasipofanya hivyo.
Ndoa ni makubaliano ya watu wawili kwa ridhaa ya wazazi ambao ndio wanatoa baraka. Mzazi asipokupa baraka hata uende kanisani hutopata hizo baraka. Na mwisho nakubaliana naye Sabato ya biblia ni siku ya Jumamosi. Kujipangia Sabato siku nyingine ni kukaidi tu na kujaribu kumfanya Mungu hajui alichokisema.
Soma kisa cha Sauli kwa nini alikataliwa na Mungu.Mungu alimwagiza akienda vitani aue kila kitu asichukue chochote.Yeye akachukua wanyama walionona ili aje amtolee sadaka Mungu.Mungu alikasirishwa na ubunifu huu wa kuvunja agizo lake kwa kubuni kitu cha kjaribu kumfurahisha.
Waliobuni jumapili waliibuni kwa ajili ya kujaribu kuifurahisha miungu yao huku wakiipamba kuwa ni siku ya ufufuko wa Kristo.Ukweli ni ubishi na ukaidi tu kumfanya Mungu hajui alichokiagiza.
Mwisho sisi sote ni wanafunzi na hatupaswi kuja na misimamo yetu ya kiimani tukiwahukumu wasioamini kama sisi. Tukubali kujifunza na kuupokea ukweli hata kama utakuumiza.