Mzee Wa Upako: Usikopeshe Mtu Hela Mpaka Roho Mtakatifu Akushukie

Mangi mmoja alikuwa anatoa sadaka kanisani. Basi akaingiza mkono mfukoni, akatoa noti ya shilingi Elfu moja akaikunjakunja akaitumbukiza kwenye kapu la sadaka. Mara ileile, kuna mzee huko nyuma akamshika bega, alivyogeuka akampa burungutu la msimbazi msimbazi, Mangi akapokea kisha akaweka kwenye kapu la sadaka. Moyoni Mangi akawa anawaza, huyu Mzee ni mcha Mungu kweli kweli, yaani wekundu wekundu wote wale katoa sadaka.

Misa ilipoisha Mangi akamfuata yule Mzee, kamwambia, "ubarikiwe sana babangu eh, leo umetoa sadaka yakutosha eh". Yule Mzee akasema, "ile sio sadaka, ni pesa zako nimekurudishia. Ulipoingiza mfukoni kutoa ile buku, lile burungutu likaanguka chini".

Mangi akili ikamruka, akamfuata Padre muda ule ule, akamwabia, "samahani sana Msee, naomba unirudishie hela yangu. Kwa kweli niliitoa kimakosa". Padre akamwambia ile pesa haiwezi kurudi kwasababu tumeshamkabidhi Mungu. Mangi akapoteza fahamu.

Ikabidi Mangi abebwe kwa Ambulance apelekwe hospitali, alipozinduka akamuona mwanamke amevaa nguo nyeupe. Mangi akasema, " Malaika afadhari tumekutana, mwambie Mungu anirudishie pesa zangu tafadhari, mimi nilizitoa sadaka kimakosa tu". Yule dada akasema, "mimi sio Malaika, mimi ni Muuguzi na hapa sio kwa Mungu, ni hospitali".
Mangi akapoteza tena fahamu.
 
kuna watu wanafanyaga biashara za kukopesha watu kwa riba maofisini na mitaani nawaoneaga huruma sana wakianza kudai wateja wao full kugombana ila hawakomiiii

mimi hela akinifata mtu naemueshimu sana kunikopa mfano laki 2 kama ninayo namdanganya sina ila namkopesha elfu 50 tu nyingine akakope kwa mwingine... namkopesha hela ambayo hata akinidhulumu sitaumia sana....

ila mambo ya kukopeshana mamilioni sijui hayo nenda bank tu ... hata uje na story gani najua muongo sababu ungekuwa mkweli benki wangekupa.. ukiona unaiogopa bank jua wewe sio msafi kwenye ulipaji madeni
 
nlimkopesha shemeji yangu 300,000 akaahidi kunilipa ndani ya mwezi, nnavyoandika hapa nina miezi 8 sijalipwa hata mia na simu zangu hapokei na sms zangu hajibu.......sikukoma rafiki yangu (mwanafunzi cbe) mwezi wa 5 kanililia shida anarudia mwaka nimkopeshe aongezee ada 200,000 afanye UE nikaingiwa huruma nikamkopesha kwa makubaliano atanilipa tena na maandishi juu, sahivi amegeuka adui yangu.

my take.......kamwe usimkopeshe mtu hela hata akija analia na kusaga meno, kama anakufa, kufa na afe. binafsi sitokuja kukopesha tena maishani bora niwape ndugu zangu au wahitaji na maskini zaidi yangu naweza kupata baraka.
 
mkuuu ela sijui ina nn, yan hata ww ukikopa , ukija kupata ,kurudisha unaona tabu flani hivi wakati ulikopa kweli.
 
mimi ukinikopa nakupa nasubr siku ya uliyoahd kurudsha, ikipta nakaa kmyaa, hapooo sikupi tena pesa.
 
kwakweli mangi alipata taabu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wale waandishi wa habari aliowatabiria kifo kisa wamemuandika kuwa alilewa wameshafariki?!
 
Unachosema ni sahihi kabisa, rafiki yangu alianza na sababu ambazo hazina mwisho, mwisho kbs akastop kujibu text na call zangu kiufupi ameua urafiki wetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…