Mzee Wa Upako: Usikopeshe Mtu Hela Mpaka Roho Mtakatifu Akushukie

Sawa nabii wa uongo tumekusikia

What goes around always comes around
 
Kwa hili namuunga mkono. Kuna mtu nilimkopesha pesa ale sikukuu ya Iddi mpaka leo hajanirudishia na mimi naihitaji hiyo pesa ila kumdai siwezi maana nilimkopesha based on humanitarian grounds... Alikuwa amesononeka sana kukosa pesa ya kula sikukuu yeye na familia yake na kwa kuwa nilikuwa na pesa nikaamua nimkopeshe... Ningejua nisingefanya hivyo...
 
Ukiijua formula ya Maisha hupati tabu kabisa.

Kamwe Usikopeshe. Ila, ili usionekane Una roho mbaya fanya hivi;

Mtu akija anashida akakuomba umkopeshe mfano elfu 50. We mwambie upo vibaya una elfu 20 tu. Mpe hiyo kama kumkopesha lakini moyoni uchukulie umempa tu. Ili usiiweke akilini na kwenye mipango yako.
Kama asipokulipa haitokuumiza na mtu huyo hawezi kuja kukukopa tena.

Hapo utakuwa unapunguza watu wa kuja kukukopa.

Note:
Huwezi kuishi kwenye Dunia hii bila kutoa msaada kwa wengine. Huwezi ona baraka, pia siku ukipata shida wewe hutapata msaada maana nawe hutoi.


sent by Samson Cyper
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…