Zee Korofi
JF-Expert Member
- Oct 5, 2021
- 1,604
- 1,430
Good afternoon brothers. Majukumu ya malezi yanakwendaje?
Uhusiano wangu na jamii;
Tangu nazaliwa na kuanza kujitambua, mzee wangu amenilea malezi ambayo naona magumu yake na athari zake muda huu. Nina 'traits' za kushangaza ila naomba mjikite kwenye kutoa ushauri na ufafanuzi tafadhali;
Mpaka umri huu sinywi pombe na sivuti sigara, sikati kona katika 'circular way', yaani ni lazima nitengeneze nyuzi karibia tisini, toka udogo nimelelewa hivyo.
Mpaka muda huu nakumbuka sijawahi kucheka, ila kutabasamu kwa sekunde zisizozidi 10. Huwa nacheka nikiwa peke yangu tu.
Huwa nalia peke yangu nikiona watoto wadogo wanakufa kwa kukosa pesa za matibabu, wanyama wanateseka n.k, huwa hata chakula hakipiti. Siku yangu huharibika kabisa.
Sili na sikumbuki kama nimewahi kula kwa watu au jirani, nimelelewa hivyo, hata nikiwa na njaa ni lazima nirudi nyumbani ndipo nile.
Nimefundishwa na mzee kutocheka hata na ndugu yangu, endapo hakuna kitu cha msingi cha kucheka, na nipo hivyo.
Nikitembea sigeuki nyuma, na nikigeuka basi ni kwa haraka mno na ni kichwa pekee tu, na siyo mwili wote. Napenda mno kufanya mapenzi.
Sijui ku'fake' kicheko au kilio, ukinichekesha hata kwa lisaa lizima, kama sijafurahi nitaishia kutabasamu tu tena kwa mbali.
Mzee amenifundisha kutoogopa yeyote hata akiwa mtu mkubwa kiasi gani, ila niheshimu kila mtu.
Haya yananitesa mno na kupelekea watu kuniogopa na kuniona kama 'maniac', hasa kwa hili la kuwa na uso mkavu na kutoigiza kicheko wala tabasamu. Nimekosa baadhi ya fursa kwa sababu hii. Mzee ameniharibu mno kwani sipendi hali hii, na ingekuwa amri yangu nisingekubali.
Hii ndiyo hali yangu halisi, sijui nitatokaje