Mzee Warioba angefaa kuwa Rais baada tu ya Mzee Mwinyi: ingesaidia kuandaa viongozi

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Kuna namna tulikosea katika mchakato wakuandaa viongozi. Wakina Mzee Warioba walipoamua kujiweka kando baada ya mwalimu kung'atuka ilikuwa kosa kubwa sana.

Nchi haikuhitaji urais wa majaribio tena bali ilitakiwa inapata viongozi kwa merits. Kinachoendelea sasa hivi toka amalize muda wake mzee Mwinyi tumekuwa tukipata viongozi kulingana na mazingira ya vita ya kisiasa yaliyopo mbele ya uwanja wa uchaguzi.

Kutokana na ukweli kwamba wanaopitishwa kuwa wagombea hawana nguvu kwa wapiga kura ndipo ikaingia kasumba kila mgombea uraisi anaaminishwa hana uwezo wakupita bila kupata backup ya dola.

Mzee Mkapa alisumbuliwa sana na Mrema hadi ikabidi mwalimu aingie kazini na yeye akakwama nakulazimisha kura za maruhani na majambia.

Mzee Kikwete alipoona Lowasa anamzidi nguvu akaweka mkakati wa kumfanya rafiki ndipo amalize kisiasa kwa kutumia dola. Vilevile kwa JPM na huko tuendako.

Ifike wakati tuanze kuandaa viongozi na kuwapa nafasi ya kujitangaza kwa umma itasaidia kufahamu nani anakubalika na kupunguza nguvu ya dola kwenye uchaguzi.
 
Labda yeye kua nje imemfanya aone vizuri zaidi.
 
Hata sasa anafaa hata kama ni kwa miezi sita tu! Kwa kipindi cha miezi sita anaweza kutupatia katiba itakayokuwa suluhisho la mengi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…