Wakuu huyu mzee wenu bila kuitaja CHADEMA hasikii raha kabisa
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, ameishutumu CHADEMA kwa kile alichodai kuwa chama hicho kimekuwa kikiwatumia vijana wa Tarime kama majeshi ya kukodi kwa ajili ya vurugu katika maeneo mbalimbali nchini.
"Kuna wakati kabla Waitara hajabatizwa, alipeleka vijana kufanya fujo, wakapata matatizo, na hata yeye mwenyewe akalazwa hospitalini. Baadaye akapona, akarudi, tukambatiza na kumpa kofia ya CCM," amesema Wasira.
Ameongeza kuwa badala ya kujiingiza katika fujo zisizo na tija, vijana wa Tarime wanapaswa kutumia fursa zilizopo wilayani humo, ikiwemo sekta ya madini na kilimo, ili kujiletea maendeleo.
"Tarime tuna rasilimali nyingi; tuna madini, wachimbaji wadogo na ardhi yenye rutuba. Tuwasaidie vijana wetu kuzitumia fursa hizi badala ya kutumiwa na wanasiasa kwa maslahi yao," amesisitiza.
Aidha, ameitaka CHADEMA kuacha mara moja kuchukua vijana wa Tarime kwa ajili ya vurugu, akisisitiza kuwa Tarime sio eneo la mapambano na vijana wake hawapaswi kukodishwa kwa ajili ya machafuko.
Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini, Mwita Waitara, amesema kuwa hatoweza kurejea Bungeni iwapo Serikali haitachukua hatua za kutatua changamoto za migogoro ya wakulima na wafugaji, miradi ya maji isiyokamilika, na hali ya miundombinu ya barabara jimboni kwake. Hata hivyo, Waitara amesisitiza...