Mzee Yussuf wa Jahazi Mahututi Muhimbili?

Mzee Yussuf wa Jahazi Mahututi Muhimbili?

Junius

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2009
Posts
3,181
Reaction score
144
Muimba taarabu mashuhuri nchini Tanzania na Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Jahazi Modern Taarab, Mzee Yusuph Mwinyi maarufu kama ‘Mzee Yusuph’, leo majira ya saa sita mchana amedondoka ghafla na kupoteza fahamu kisha kukimbizwa katika Hospitali kuu ya Taifa ya Muhimbili.

Tukio hilo la kushtukiza limetokea wakati Mzee Yusuph akiwa katika ofisi za Radio Clouds FM, jijini Dar es Salaam alikokuwa amekwenda kwa shughuli zake za kikazi. Akiwa mapokezi(Reception), ghafla hali yake ilianza kubadilika na akaanza kulalamika kuwa anasikia kizunguzungu kabla ya kudondoka chini na kupoteza fahamu.

Kwa sasa yuko Hospitalini Muhimbili na madaktari wanahangaika kuyanusuru maisha yake.


source:Global Publishers Ltd
 
Tunajaribu kuwasiliana na ndugu wa karibu kujua kinachoendelea...wadau tusaidiane mlioko karibu uko.
 
Muimba taarabu mashuhuri nchini Tanzania na Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Jahazi Modern Taarab, Mzee Yusuph Mwinyi maarufu kama ‘Mzee Yusuph’, leo majira ya saa sita mchana amedondoka ghafla na kupoteza fahamu kisha kukimbizwa katika Hospitali kuu ya Taifa ya Muhimbili.



Du , Mkuu ulivyoripoti imenitisha sana mimi...Kwamba yu mahututi si jambo la mchezo mkuu!...
Mungu mwenyezi amrudishie afya yake kiumbe huyu, na aendelee na shughuli zake!
 
source:Global Publishers Ltd

NO COMMENTS
 
Mbona taarifa nilizozipata anadaiwa yupo TMJ na amerejewa na fahamu na kaanza kuzungumza ?
 
tena ndo zao-nadhani alasiri ya leo wakubwa au? Ahahaaaa
 
Duh Mungu amnusuru tuendelee kulamba
Haya sasa...ndo haya yanaanza kujitokeza taratibu!!1
Jamani, kwasasa ni mgonjwa, tunachotakiwa kufanya ni kumwombea tu, apone..
Habari za kumlamba zitulie kwanza!
 
JAMANI............y.....kwa nini?mola amjaalie jamani MFALME MBONA KULALAA....aaa sijalalaa nautia kasiiiii
 
Mfalme ameruhusiwa aliwekwa mapumzikoni TMJ na sio Muhimbili tumeongea nae sasa hivi mashabike wake msitie hofu.
 
Mungu amponye haraka maana nasikia kifupi ndugu wameshaana kungangania funguo za gari lilipo hapo nje hospt
 
Back
Top Bottom