Mzgu aliniuliza 'What can I do for you?'

Mzgu aliniuliza 'What can I do for you?'

Tata ya bana

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2018
Posts
295
Reaction score
357
Wakuu za jioni.

Nilikutana na mzungu mmoja mwanaume katika cafe moja tukakaa meza moja tukapiga story huku tunakunywa kahawa, tuliongea mengi kuhusu maisha na yeye alijieleza ni doctor kule Machame wa kujitolea. Baadaye akawa anaaga ila akaniambia "WHAT CAN I DO FOR YOU"? nilielewa maana yake ila nilishindwa kujibu zaidi nilimuaga na kupeana business cards kiuhalisia nilitakiwa nimpige mzinga au?

Nilijiona fala sana
 
What can I do for you?

Kwa kadri ya uelewa wangu, ungetakiwa kujibu kutokana na mazungumzo mliyokuwa mnayazungumza kwa wakati huo.

Mfano; kama ulikuwa unamuelezea juu ya hali yako ngumu ya kimaisha basi ungetakiwa kumueleza ni kwa namna gani angeweza kukusaidia ili hali hiyo itengamae

Kama mlikuwa mnazungumza juu ya nia yako ya kusafiri kwenda nje, basi umuambie ni kitu gani angeweza kukusaidia. Labda, jinsi ya kupata visa, taarifa muhimu jinsi ya kufanikisha, mahali pazuri pa kufinikia, nk.

Au labda mazungumzo yalikuwa njia ya kukutana na wachuchu wa huko kwao. Basi angekupa hints za kufanya.

Haimaanishi kukusaidia kifedha kama unavyowaza.
 
Back
Top Bottom