SoC02 Mzigo mliomtwika Mama Tanzania ni mkubwa mno

SoC02 Mzigo mliomtwika Mama Tanzania ni mkubwa mno

Stories of Change - 2022 Competition

Deodravis

New Member
Joined
Jul 27, 2022
Posts
2
Reaction score
0
Na Deodravis

Mtume Yohana Alizoea kusimama katikati Yao bila woga aliwapinga hoja zao, aliyekuwa msaidizi wake akiwa kusini, mtendaji wake mkuu akiwa kasikazini, basi yeye atakuwa magharibi. Kila kitu upande wake kilikua demokrasia inayokuja kisha inakataa. Lakini mama Tanzania Wengi walisema kabebeshwa mizigo ya uhapa wa fedha mtaani na ufinyu wa demokrasia. Kila mtu alisema wengine ndio hawakuona hata zuri moja.

Tujadili hapa. Je ni kweli Yametimia yaliyonenwa nae. Eti Mimi ni mtumishi wenu na mtanikumbuka. Umma wa mujini hata vizazi vya vijijini. Wadogo Kwa wakubwa Viongozi Kwa vigogo kilichobaki Sasa Kila mmoja anadeka Kwa Mama. Hakika kumbukwe zaburi "Nani kama Mama".

Kero za wana-Jelusalem zimegubikwa tu sifa Kwa mama. Bei za bidhaa zinapanda Mama anaupiga mwingi. Deni la taifa laongezeka ni mama anaupiga mwingi. Miradi ya maendeleo inasua sua kukamilika ni mama anaupiga mwingi. Wanaosema anaupiga mwingi ndio wale wale waliokosoa hata kile kizuri Cha mtume. Ingawa haimaanishi hakuwa na mapungufu.

Mama Tanzania atia huruma nilimwona akitembea taratibu toka uchumi wa chini kwenda uchumi wa kati. Aliahidiwa mengi akisisitizwa kuifanya kazi. Lakini sitamani kumtazama Tena Kwa maana nitamuonea huruma na japo Sina uwezo wa kumsaidia mimi ni kijana mdogo. Mama Tanzania katwikwa Mzigo mzito na wanae ndio wanashangilia na wanamlazimisha aseme Wala sio mzito.

Kwenye fulushi alilobeba mama Tanzania Kuna tozo, Bei ghali, Ufisadi, urasimu ulioanza kurudi Tena kwenye ofisi za umma ambao ulikua umepungua kipindi Cha mtume, ingawa tulitegemea mikopo na baadhi ya misaada ingesaidia Mzigo huu lakini bado hakuna anaekemea Wala kuhoji kila mtu "Mama anaupiga mwingi"

Hata waliojiita wayahudi niliowaamini nikawaona miamba ya babeli, Tena iliyomikuu yeyote atakae anguka juu yake anasagikasagika. Sasa limekua jiwe butu la kusugulia miguu ya mwanamwali lisilotakatisha. Hakuna kinachopingwa, wamekosa hoja na wao wanarumbana tu wenyewe.

Eeh Mungu wa Tanzania ninakuomba watekekeze Hawa waliomtwisha mama Tanzania Mzigo huu mkubwa.

Siyo Kwa chuki Wala husuda ila huo mpira unaosemekaka unapigwa mwingi si biriani Tena. Ni pira joro la Zanzibar. Wanaosifia wanalinda nafasi na ulaji wanaoumia wapo wanachekelea.

"Let's this be the story of Change"
IMG_20220813_095355_798.jpg
 
Upvote 0
Back
Top Bottom