Mziki wetu Unaangushwa Na "Beats" Na Sio "Mashairi wala Videos"

Mziki wetu Unaangushwa Na "Beats" Na Sio "Mashairi wala Videos"

Traveller X

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2017
Posts
271
Reaction score
305
Mnaweza mkanikosoa tu wadau lakini nimekua na naendelea kufatilia kukua na kushuka kwa mziki wetu "BongoFlava" lakini pia nafatilia sana mziki kutoka "Nigeria" SouthAfrica" pamoja na huko "Mbele" na kwa kipindi cha mwanzo nlikua nahisi pengine ni "Lugha" yetu ndo inatufanya tusipenye zaidi kwenye nchi nyingi za afrika na duniani lakini nkagundua hapana sio lugha kwasababu kuna nchi wanaongea lugha hata hazieleweki lakini mziki wao unachezwa na kusikilizwa duniani kote sasa kwanini huu wabongo haupenyi huko mbele kulinganisha na mziki wa south africa na nigeria?

Pengine ni mashairi? Lakini hapa napo nkaja kugundua kua bongo kuna watu wanajua kupanga mashairi vizuri kuliko hata hao wanigeria sasa kwanini hatutoboi kwa wingi? chukulia nyimbo ya Davido hii mpya inaitwa "Fall" sikiliza kwa makini mashairi yake yani ni vitu vya kawaida tu anaongea humo ndani, "Mara banana follow you" yani vitu vya ajabu tu

Alaf njoo linganisha na ngoma labda ya "Ben Pol" tu "Moyo Mashine" ambayo ukiskiliza mashairi nikweli yamepangwa na yakapangika

Sasa kwanini ya ben pol haijatoboa afrika nzima kama hii ya davido inavyozidi kutoboa??

Bado naendelea kujiuliza lakin nilichogundua kwa haraka haraka ni "BEATS" zinatuangusha sana tena sana,Wanaigeria wanabebwa kwa asilimia 90 na beats zao na kusema ukweli wanajua kutengeneza beats zikakufanya ucheze tu hata kama hutak,

Chukulia mfano mdogo tu wa hii ngoma ya underground wa nigeria inaitwa "Gimme Love" ya dogo mmoja anitwa "ryan" isikilize hyo beat utasema jamaa ni bonge la star kumbe ni underground tu lakini hyo beat ni balaa

Alaf njoo kwa underground wetu huku utakuta ana mashairi mazuri tu lakini kwa hizi beat zetu inakua kazi yote ni zero tu

Kwangu mimi naona tatizo liko kwa ma Producer wetu hawatupi vitu ambavyo vinashawishi kila mtu kusikiliza, Sijajua kwenu nyie wadau mnaona tatizo liko wapi????
 
Mkuu em soma tena kwa makini ulichopost...
 
Mimi nmekuelewa.
unachokifikiria nakupa 100% hata mimi ..
wapopo wana beatz.[emoji122][emoji122][emoji122]
nawaambiaga watu humu Daily kuwa hakunaga wakiimbacho hao wenzetu sio west Africa wala majuu,
Lakini beatz zinawabeba mno, na ndio mziki,unadhani Darasa asingepigiwa Muziki na Ttouch ungehit?
kwanini My number one ya Diamond haichujagi? beats!! Nyimbo nyingi za diamond zimehit kipindi cha nyuma kwasababu perfect beatz,nk

sasa sielewi wasanii wetu hawalioni hili[emoji24][emoji24]
Video nzuri bila wimbo mzuri ni bure,Japo kwa videos tunajitahidi.
Hata hapa tuna producers wazuri tu lakini sio wa kuwategemea sana, lazima wasanii wetu wavuke ng'ambo kutafuta fursa.

Wenye masikio na wasikie ; nikianza na wcb lizer tumemchoka!!!!!!!!!!!!!!
 
Nadhani toka umeingia jamii forums hili itakuwa post ilio legit toka kwako kuliko nyinginezo zote. Nishasemaga mziki ili uwe mzuri lazima production iwe nzuri...ni lazimaaaa!!!

Beats iwe inavutia kusikiliza kama si kuchezeka pia iwe mastered vizuri isiwe na kelele sana zinazoweza chosha kusikiliza.

Kwa sasa BigStrongSound ndio producer anaetisha kwa ku drop hits za Nigeria...Nyimbo kama IF ya Davido, sikiliza YAWA ya Tecno, RARA, DIANA utaona jinsi beat inavyoweza kufanya track iwe hit song.

Kwa Bongo recently T.Touch ana mkono mzuri wa kufanya hits bila kumsahau producer LUFFA.

Kwa T.Touch sikiliza Furaha ya young dee, Muziki ya darasa, Kiboko ya Mabishoo ya harmo rapa, Muziki ya darasa, Saka hela ya Ney wa mitego, bongo bahati mbaya n.k

Luffa sikiliza production ya Waya ya weusi, Juu ya jux na vanessa, Sina koloni ya Motra, Your body ya Godzilla na Maua sama, Go low ya jux na G nako n.k

Manecky kwake sikiliza, Nina imani nyimbo flani ambayo jux kashirikishwa, Acha niende ya Baraka d prince,Samboira ya ben pol, Sisikii jux, nyimbo nyingi za diamond za album ya kamwambie, nyimbo za mirror n.k

Nahreel pia ni mkali wa beats zinazofanya mziki mzuri anakaribiana na luffa kwa kiwango ni maarufu zaidi kuliko luffa...sikiliza Nobody ya vanessa mdee, Nusu Nusu ya weusi, Game ya navy kenzo, don't bother weusi, Safari ya weusi.

Ukiskiliza hizo productions utapata kuelewa beats zina nguvu kiasi gani katika kuifanya nyimbo idumu katika ubora wake hata baada ya kuchuja kwenye top charts za redioni/tv stations. Na hapo ndipo hasa wabongo tunapokoseaga
 
100% true, alafu maproducer wengi wanarudia biti alafu wanaongezea vitu vidogo.
 
Nimekuelewa sana mkuu.

On point.
 
FL studio inatosha kwa producer wa tanzania hawasumbui vichwa
Unalosema ni kweli ebu ona huyu kija siyo producer ka remake beat ya mask off siyo kwa kutumia softwares
Future - Mask off (instrumental):
 
Umenenena vitu vya maana sana midundo yetu bongo ni ya kishamba sana
 
Mimi nmekuelewa.
unachokifikiria nakupa 100% hata mimi ..
wapopo wana beatz.[emoji122][emoji122][emoji122]
nawaambiaga watu humu Daily kuwa hakunaga wakiimbacho hao wenzetu sio west Africa wala majuu,
Lakini beatz zinawabeba mno, na ndio mziki,unadhani Darasa asingepigiwa Muziki na Ttouch ungehit?
kwanini My number one ya Diamond haichujagi? beats!! Nyimbo nyingi za diamond zimehit kipindi cha nyuma kwasababu perfect beatz,nk

sasa sielewi wasanii wetu hawalioni hili[emoji24][emoji24]
Video nzuri bila wimbo mzuri ni bure,Japo kwa videos tunajitahidi.
Hata hapa tuna producers wazuri tu lakini sio wa kuwategemea sana, lazima wasanii wetu wavuke ng'ambo kutafuta fursa.

Wenye masikio na wasikie ; nikianza na wcb lizer tumemchoka!!!!!!!!!!!!!!
Lizer kiukweli hata mie nimemchoka skuizi hata sishtuki kiivo wcb wakitoa nyimbo.
 
Nakubariana na mtoa mada, ila beat pekee haiwezi ikafanya msanii akatoboa, kuna Melody, Vocal n.k...
By the way Beat ndo kitu inamvuta msikilizaji toka nyimbo inaanza....
Mm napenda sana hizi nyimbo 2 mpya za Davido, If na Fall....Beat, Melody, Vocal na Mashairi vyote vinanikosha..
 
Kingine ni aina ya wasanii tulionao...hatuna wanamuziki.

Mathalani, unategemea wengi waimbe nyimbo zinazoishi ila ni ngumu kupata ya aina hiyo.

Zile sauti zenye identity ya mtu hakuna, kama ukisikia sauti ya W.Houston na jinsi anavyocheza na sauti kwenye nyimbo zake, unaona achilia mbali mashairi na beats, kuna zaidi ya hivyo vitu vitakavyokufanya useme Daaaaamn......binti/kijana yule ameimba aiseee.

Naombeni jina la mbongo fleva mwenye angalau robo ya uwezo wa watu hao kimuziki na wimbo huo utakaoona umetisha.
 
Back
Top Bottom