Mzimu wa Richmond warejea bungeni leo katika mjadala wa gesi asilia

Mzimu wa Richmond warejea bungeni leo katika mjadala wa gesi asilia

Paparazi Muwazi

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2007
Posts
310
Reaction score
80
Mzimu wa Richmond leo umejitokeza kwenye mjadala bungeni kuhusu utekelezaji wa maazimio 26 ya Bunge juu ya gesi asilia. Aliyerejesha kwa kishindo mzimu huo ni mbunge wa Ubungo John Mnyika ambaye alidai kuwa maazimio ya bunge kuhusu gesi asilia hayana tofauti na yale yaliyopitishwa mwaka 2008 kuhusu Richmond ambayo mpaka sasa hayajatekelezwa. Ametaka serikali ieleze hatua ambazo imechukua kwa Waziri na watendaji wote waliohusika na ufisadi katika gesi asilia. Amedai kuwa iwapo hatua hazitachukuliwa mpaka mwezi Aprili mkutano ujao bunge litangaze mgogoro na serikali na lichukue litumie mamlaka kwa ibara ya 63 ya katiba.

Mbunge mwingine aliyeupokea mzimu huo ni Mbunge wa Kibondo Felix Mkosamali ambaye alisema kwamba bunge limepoteza uwezo wa kuisimamia serikali kwa kuwa maazimio ya Richmond hayajatekelezwa. Mkosamali ametaka maafisa wote waliofanya uzembe katika gesi asilia ikiwemo waliojadili mikataba waweze kuchukuliwa hatua za kinidhamu na kisheria. Mzimu huo wa Richmond ulielekea pia kumkumbuka Mbunge wa Bariadi John Cheyo ambaye alisema kuwa mtindo wa kuunda kamati za bunge ni mzuri lakini akataka hatua kuchukuliwa kama ilivyokuwa katika kashfa ya Richmond. Mzimu huo unatarajiwa kutawala bunge jioni wakati mjadala kuhusu utekelezaji wa maazimio ya bunge kuhusu gesi asilia utakapoendelea.

Soma
 
tunataka hoja binafsi ya mnyika ijadiliwe ili haya yote yawe wazi kwa sababu inaonekana wabunge ni wapiga kelele tu wakati kwa upande wa serikali ndiyo wanaonekana wazembe
 
tunataka hoja binafsi ya mnyika ijadiliwe ili haya yote yawe wazi kwa sababu inaonekana wabunge ni wapiga kelele tu wakati kwa upande wa serikali ndiyo wanaonekana wazembe

Tumeshtukia mkakati wa CHADEMA kumchafua Lowassa, hiyo hoja wanaCCM hatuikubali. Mtaishia kwenye huu mjadala wa gesi tu, Richmond hamfiki

..........ndiyohiyo
 
Tumeshtukia mkakati wa CHADEMA kumchafua Lowassa, hiyo hoja wanaCCM hatuikubali. Mtaishia kwenye huu mjadala wa gesi tu, Richmond hamfiki

..........ndiyohiyo
Hivi unaweza ukamchafua bata??

I am just thinking.....
 
Tumeshtukia mkakati wa CHADEMA kumchafua Lowassa, hiyo hoja wanaCCM hatuikubali. Mtaishia kwenye huu mjadala wa gesi tu, Richmond hamfiki

..........ndiyohiyo

Jibu nikwamba, huwezi kumchafua mtu aliyechafuka. niwakati wake wakujisafisha kama alikuwa amechafuka.
 
kweli kabisa huwezi kuupata ukweli ndani ya wongo,ingawa unaweza kupata uongo ndani ya ukweli",chedema fanyeni kazi bana
 
Back
Top Bottom