Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,925
MRADI wa ujenzi wa Bwawa la Kawa lililoko katika Jimbo la Nkasi Kaskazini, uliotekelezwa na Wizara ya Maji umeibua utata mkubwa baada ya kubainika kuwa bwawa hilo limejengwa katika eneo linalomilikiwa na mwekezaji, Mbunge wa zamani wa Jimbo la Kwela, Dk. Chrisant Mzindakaya.
Utata huo uliwekwa hadharani hivi karibuni pale Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ilipotembelea Makao Makuu ya Wizara ya Maji jijini Dar es Salaam ili kuangalia mikakati ya Wizara hiyo katika kutatua kero ya maji nchini. Hatua hiyo ilimfanya Mwenyekiti wa Kamati hiyo, John Cheyo ambaye ni Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), kuwa mbogo akitaka kujua ni kwa vipi, Wizara hiyo iliidhinisha ujenzi wa bwawa wakati ikijua kuwa eneo hilo ni shamba la Dk. Mzindakaya.
Katika majibu yake, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Sayi alisema kuwa wizara yake ilijenga mradi huo bila kujua kuwa eneo hilo ni la mwekezaji na kukiri kuwa ni kosa kubwa kwa wizara kufikia uamuzi wa kujenga mradi mkubwa kama huo bila kujua uhalali wa eneo husika. Hata hivyo, Mbunge wa Nkasi Kaskazini ambako ndiko mradi huo ulipo, Ally Kessy Mohammed (CCM) alieleza kutokukubaliana na utetezi huo wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, kwamba wizara hiyo ilijenga mradi huo bila kufahamu juu ya uhalali wa eneo husika. Mwenyekiti si kweli kuwa Wizara haikuwa ikijua kuwa eneo hilo ni la mwekezaji. Kama kweli Wizara ilikuwa haijui kuwa eneo hilo ni ranchi ya mwekezaji, kwanini bwawa likajengwa katika eneo lisilofaa?
Nasema hivyo kwa sababu usambazaji wa maji kutoka katika bwawa hilo kwenda kwa wananchi ni mgumu sana, lakini ni rahisi sana kusambaza maji hayo katika ranchi hiyo ya Dk. Mzindakaya, alihoji Kessy. Mbunge huyo alisema mradi huo ulioigharimu serikali Sh bilioni 1.1, ulilenga kutoa huduma ya maji katika vijiji vya Nkundi, Kalundi na Fyengereza, ingawa pamoja na mradi huo kukamilika lengo lake la kuhudumia vijiji hivyo limekwama kutokana na utata uliojitokeza. Mheshimiwa Mzindakaya anadai fidia ya mradi huo kujengwa katika ranchi yake ili aweze kuwaruhusu wananchi kutumia maji hayo wakati serikali imetumia mamilioni ya shilingi kuugharamia kwa ajili ya kuwasaidia wananchi.
Sakata hili limesababishwa na Mzindakaya kwa sababu, akijua kuwa eneo hilo ni lake na shughuli yake kubwa ni ufugaji alipeleka ombi serikalini kuomba mradi huo kujengwa katika eneo lake kwa ajili ya vijiji hivyo huku Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi ikiwa haijui lolote. Sasa ikiwa alipeleka ombi hilo kwa ridhaa yake mwenyewe kuruhusu ujenzi wa bwawa la Kawa katika ranchi yake, kwanini anawazuia wananchi kutumia maji hayo?
Ikiwa hiyo ndiyo hali halisi kwanini anadai fidia serikali wakati ombi la ujenzi wa bwawa hilo alilitoa mwenyewe. Zaidi ya hayo Mbunge wa zamani wa Nkasi Kaskazini, Ponsiano Nyami aliwahi kutoa taarifa bungeni juu ya hatari iliyopo ikiwa mradi huo mkubwa utajengwa katika ranchi hiyo, lakini kwa bahati mbaya wizara haikuchukulia manani tahadhari hiyo na iliendelea na mipango yake ya ujenzi, alisema Mbunge Kessy..............
Source: Habari Leo