Mzize achaguliwa kuwa mchezaji bora wa CAFCL

Analog

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2024
Posts
323
Reaction score
618
Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Yanga, Clement Mzize (20) amechaguliwa na shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) kuwa mchezaji bora wa wiki baada kuisaidia Yanga kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya TP Mazembe kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Katika mchezo huo, ilishuhudiwa Yanga ikitoka nyuma na kupata ushindi ambapo Mzize alipachika mabao mawili kati ya matatu yaliyofungwa huku akionyesha kiwango bora. CAF imemtangaza Mzize baada ya kuwashinda nyota wengine waliokuwa wakichuana kwenye orodha ya wachezaji waliofanya vizuri wiki hii.

Mabao mawili alioyafunga dhidi ya Mazembe yanamfanya kufikisha jumla ya mabao matatu kwenye mshindano haya msimu huu baada ya kucheza mechi tatu.

Mzize ambaye ameonyesha kiwango bora kwenye mchezo uliopita anaendelea kuvivutia Vilabu vikubwa hapa Afrika ambavyo vimekuwa vikiitaji huduma yake.

Yanga inashika nafasi ya tatu kwenye kundi A ikiwa na pointi nne, nyuma ya MC Alger iliyo nafasi yapili kwa pointi tano na vinara Al Hilal wenye pointi 10, timu inayoburuza mkia ikiwa ni TP Mazembe ambayo ina pointi mbili.

Mchezo unaofuata Yanga itasafiri kwenda Maurtania kuwakabili Al Hilal ya kocha, Florent Ibenge katika mchezo utakaopigwa Januari 12, 2025.

Yanga inaingia katika mchezo huo ikiwa na kisasi cha kulipa baada ya kupoteza mechi ya nyumbani iliyopigwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo ilichapika mabai 2-0.

Iwapo Yanga itapata ushindi dhidi ya Al Hilal itajiweka pazuri kufuzu hatua ya robo fainali kwani itahitaji kushinda mechi yao ya mwisho ya nyumbani dhidi ya MC Alger Januari 18, 2025

operanews1736360859653.jpg
 
View attachment 3196176
Makolo wanaumia sana utazani tumechukua ubingwa
 
Tunatamani tuwe wazalendo kumsupport ila.....
 
Hongera sana kijana Mzize. Ingawa mimi ni mwana Simba lakini sina budi kukupongeza kwa kutuwakilisha vema Tanzania.
Hivi sasa nchi yetu ina mastaa wengi wa kigeni lakini kuteuliwa kwako kumeionyesha Dunia kuwa kwenye soka la Tanzania kuna watu.
Naamini kwa uwezo ulionao ungekuwa mchezaji wa kigeni ungeoga mapesa ya Yanga, lakini utanzania wako unawafanya wakubwa hapo Jangwani wakupuuze.

Huu ndiyo muda wako wa kutafuta maokoto nje ya Tanzania.
Tafadhali usiige akili za Mrisho Ngasa.
Pesa kwanza mapenzi baadaye.
 
Back
Top Bottom