Mshambuliaji wa Yanga, Clement Mzize amesema ubora wa pasi ya mwisho ya Clatous Chama ulimpa urahisi wa kukwamisha mpira nyavuni.Mzize alifunga bao la nne na la mwisho kwenye ushindi wa mabao 4-1 ilioupata Yanga dhidi ya Azam katika fainali ya Ngao ya Jamii iliyochezwa juzi Jumapili kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam. Mabao mengine yalifungwa na Prince Dube, Yoro Diaby (alijifunga) na Stephane Aziz Ki. Bao la Azam lilifungwa na Feisal Salum 'Fei Toto'.
Akizungumza na Mwananchi, Mzize amesema kabla ya kuingia uwanjani akitokea benchi, Kocha Miguel Gamondi alimtaka kuhakikisha anatumia nguvu zote kupeleka mashambulizi kwa wapinzani na ndicho alichokifanya.
"Alinionyesha mianya mingi ya kupita na kunisisitiza kutumia nguvu na akili kusogeza mashambulizi kwa wapinzani ndicho nilichokifanya, bao nililofunga nilianza kulitengeneza mwenyewe kwa kukokota mpira kutoka eneo la mbali la uwanja," amesema na kuongeza;