Mzize ni bora zaidi Kuliko Elie Mpanzu, miles ahead kulingana na uchambuzi huu

ubarinolutu

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2012
Posts
2,424
Reaction score
4,954
Kwanza kabisa hawa wote ni vijana wadogo, Elie Mpanzu ana miaka 22, na Mzinze ana miaka 22, Kiuhalisia Mzize ana mafanikio makubwa sana kuliko mpanzu, hata ubora wa uwanjani bado Mzize yupo juu, hapa chini ni strength zao, sasa angalieni nani fundi:

1. Scoring capability (Uwezo wa Kufunga): Katika sekta hii mzinze yupo juu kwani ukilinganisha takwimu za Mpanzu na Mzize katika misimu miwili iliyopita, Mzize ana magoli mengi kuliko elie Mpanzu.

2. Aerial Threat (Uwezo wa Kucheza na Kichwa): Mzize ni 6ft tall, wakati Mpanzu ni 5 FT 6 inches Tall (Mbilikimo), katika mipira ya kucheza na kichwa mzize amemzidi mbali sana elie Mpanzu, na ameshafunga magoli mengi sana ya kutumia kichwa, kwakuwa ni jitu refu kama Lijerumani.

3. Nguvu/Strengh: Mzize ni jitu lenye miraba minne, na limeenda juu, elie mpanzu ni mfupi wa kimo na hana nguvu kufikia za mzize.

4. Left foot/right foot combined strenght (Uwezo wa kutumia miguu yote): Katika hili ya uwezo wakutumia miguu yote , Mzize amemuacha mbali sana Mpanzu, ni hiv Mpanzu ni predominantly anatumia mguu wa Kulia, wakati mtaalamu Mzize anatumia miguu yote miwili, kitu ambacho ni wachezaji wachache sana wana baraka hiyo , mfano Carzola, Zidane, Rosicky, Mzize ana wezakudribble kwa miguu yote miwili.

5. Speed /Kasi: Katika Hili bado mzize anamzidi mpanzu, kwakuwa Mpanzu anasifika kuwa na quick short busrt of speed au acceleration kama aliyokuwa nayo messi, lakini Mzize na ana speed kubwa kama aliyokuwanayo ronaldo na mbappe, au alfonso daves, ukitaka kujua hili kaulize uwanja wa mazoezi wa Yanga.

6. Football Skills: Hapa Bodaboda; Mzize anakalishwa kiukweli Mpanzu ni mtu aliyejaaliwa skills za mpira ni hatari katika sekta hiyo.

7. Football IQ: Hapa bado mpanzu anaendelea kuwa juu, kumzidi boda boda Mzize, Mpanzu amejaaliwa football IQ Kubwa.

8. Defensive Ability/ Uwezo wa kuzuia: Hapa Ukweli ni kuwa mzize ni mkabaji mzuri mbali sana kuliko Mpanzu, hivyo katika nyanja hii ya kuisaidia timu kuzuia bado mzize yupo Juu.

Kufuatia vipengele nane hapo juu vilivyochambuliwa kitaalamu na kwa kuangalia uwezo wa kila mmoja bila kumpendelea, nakiri kusema kati ya vipengele nane muhimu Mzize ameibuka juu katika vipengele 6 na Mpanzu ameibuka juu katika vipengele 2; Hivyo kiuwezo Mzize yupo juu kwa Asilia 75 wakati Mpanzu yupo juu kwa asilimia 25 tu.

Hivyo tuendelee kusubiri mpaka tarehe 10/08/24 tuone kama Elie Mpanzu atatangazwa kujiunga na Club yoyote hapa na most likely atajiunga Simba au Yanga sioni club nyingine ambayo atajiunga.

Nitaleta Post ingine ya Kulinganisha Uwezo wa Winga Kibu Denis, na Max Mpia Nzengeli.
WhatsApp-Image-2022-12-18-at-3.37.36-PM.jpg
 
Vitu viwili ni muhimu zaidi, na hapo kwa ulivyoandika basi mpanzu ni bora zaidi.

1.football IQ
2. SKILLS.

mzee ukiwa na vitu hivyo viwili muhimu na mwenzako hana, basi ili awe mzani sawa na wewe atahitaji sifa za ziada karibia 10 hivi.. Sijui urefu, kukaba, kujituma, speed, kucheza nafasi zaidi ya moja, kutumia miguu yote, nidhamu uwanjani, etcetera.
 
kati ya vipengele nane muhimu mzize ameibuka juu katika vipengele 6, na mpanzu ameibuka juu katika vipengele 2. Hivyo kiuwezo mzize yupo juu kwa Asilia 75 wakati mpanzu yupo juu kwa asilimia 25 tu.

Inawezekana Yanga walikuwa wanahitaji la mtu mwenye uwezo wa kufanya hivyo vitu vya 25% pekee...
 
Katika usajili ambao umeniuma ni Yanga kutomchukua yule Kipre wa Azam, Azam wamemwachia kwa pesa ndogo sana sikutegemea kabisa. Hiyo pesa hata Yanga ingemudu kuitoa kwa Azam.
 
Sijui ilikuaje tukamkosa ila Kipre na Chama au Musonda bora Kipre maana tuna strikers wa kutosha.
 
Simba ndo angeweza kwenda, Yanga pale namba asingepata
Huyu ni winga, sasa pale Yanga kuna mawinga wangapi wa maana? Gamondi analazimika kuwatumia Musonda na Mzize muda mwingine kama mawinga hasa baada ya Skudu na Okrah kutokuwa na msaada. Kwa Tanzania hakukuwa na winga hatari kama Kipre jamaa ana kasi, anapiga chenga na ana uwezo wa kufunga. Pale Yanga ni winga yupi anayeweza mfikia?
 
Maxi Mpia Nzingeli
 
Katika usajili ambao umeniuma ni Yanga kutomchukua yule Kipre wa Azam, Azam wamemwachia kwa pesa ndogo sana sikutegemea kabisa. Hiyo pesa hata Yanga ingemudu kuitoa kwa Azam.
Yule alifosi kuondoka azam na walipojua anataka kwenda Yanga ndio wakamuuza,ila ingekua Yanga wasingemuuza kwa bei ile
 
Mzize ni mchezaji mzuri mno na hatari kuliko danger atafika mbali akiwa makini zaidi na mazoezi ya kutosha, anatakiwa kufanyia kazi mambo manne ili kuwa tishio hapa bongo na Africa.

1. Mzize anatakiwa kuwa na precision wakati wa kulenga lango, akiwa ndani ya box na kuamua kupiga mpira atulie na kupiga boli sehemu anayotaka yeye mpira uende na si kupiga mpira tu kama kichaa. Papara kibao za nini? Kila siku anapaisha mipira tu anatuboa sana mashabiki, mipira kumi anayopiga kwa kukurupuka goli moja tu!!

2. Ajifunze kuangalia kwa haraka wenzake walio na nafasi nzuri ya kufunga awape pasi sio kulazimisha kufunga hata pale nafasi ikiwa haipo. Hata assist inahesabika mshambuliaji umefanya kazi nzuri. Aweke maslahi ya timu mbele.

3. Anatakiwa kujua hayuko peke yake uwanjani anapoenda mbele kwa kasi na mpira awe pia anaangalia wenzake walipo ili kuomba msaada inapobidi ili kutopoteza mipira ovyo.

4. Ajifunze kulazimisha kuingia na mpira ndani ya box ili tupate penati nyingi makolo na wengine wakimchezea rafu, Djuma Shabani alikuwa na uwezo huo anaenda pembeni na mpira kwa kasi kisha anaingia ndani ghafla lazima umchezee rafu. Striker lazima ulete faulo na penati nyingi wapigaji wapo kama Chama, Ki Aziz etc.
 
Ila hili la uchoyo siku hizi kapunguza maana anatoa assist Sana.
 
Kwanza kabisa hawa wote ni vijana wadogo, Elie Mpanzu ana miaka 22, na Mzinze ana miaka 22, Kiuhalisia Mzize ana mafanikio makubwa sana kuliko mpanzu, hata ubora wa uwanjani bado Mzize yupo juu, hapa chini ni strength zao, sasa angalieni nani fundi:

1. Scoring capability (Uwezo wa Kufunga): Katika sekta hii mzinze yupo juu kwani ukilinganisha takwimu za Mpanzu na Mzize katika misimu miwili iliyopita, Mzize ana magoli mengi kuliko elie Mpanzu.

2. Aerial Threat (Uwezo wa Kucheza na Kichwa): Mzize ni 6ft tall, wakati Mpanzu ni 5 FT 6 inches Tall (Mbilikimo), katika mipira ya kucheza na kichwa mzize amemzidi mbali sana elie Mpanzu, na ameshafunga magoli mengi sana ya kutumia kichwa, kwakuwa ni jitu refu kama Lijerumani.

3. Nguvu/Strengh: Mzize ni jitu lenye miraba minne, na limeenda juu, elie mpanzu ni mfupi wa kimo na hana nguvu kufikia za mzize.

4. Left foot/right foot combined strenght (Uwezo wa kutumia miguu yote): Katika hili ya uwezo wakutumia miguu yote , Mzize amemuacha mbali sana Mpanzu, ni hiv Mpanzu ni predominantly anatumia mguu wa Kulia, wakati mtaalamu Mzize anatumia miguu yote miwili, kitu ambacho ni wachezaji wachache sana wana baraka hiyo , mfano Carzola, Zidane, Rosicky, Mzize ana wezakudribble kwa miguu yote miwili.

5. Speed /Kasi: Katika Hili bado mzize anamzidi mpanzu, kwakuwa Mpanzu anasifika kuwa na quick short busrt of speed au acceleration kama aliyokuwa nayo messi, lakini Mzize na ana speed kubwa kama aliyokuwanayo ronaldo na mbappe, au alfonso daves, ukitaka kujua hili kaulize uwanja wa mazoezi wa Yanga.

6. Football Skills: Hapa Bodaboda; Mzize anakalishwa kiukweli Mpanzu ni mtu aliyejaaliwa skills za mpira ni hatari katika sekta hiyo.

7. Football IQ: Hapa bado mpanzu anaendelea kuwa juu, kumzidi boda boda Mzize, Mpanzu amejaaliwa football IQ Kubwa.

8. Defensive Ability/ Uwezo wa kuzuia: Hapa Ukweli ni kuwa mzize ni mkabaji mzuri mbali sana kuliko Mpanzu, hivyo katika nyanja hii ya kuisaidia timu kuzuia bado mzize yupo Juu.

Kufuatia vipengele nane hapo juu vilivyochambuliwa kitaalamu na kwa kuangalia uwezo wa kila mmoja bila kumpendelea, nakiri kusema kati ya vipengele nane muhimu Mzize ameibuka juu katika vipengele 6 na Mpanzu ameibuka juu katika vipengele 2; Hivyo kiuwezo Mzize yupo juu kwa Asilia 75 wakati Mpanzu yupo juu kwa asilimia 25 tu.

Hivyo tuendelee kusubiri mpaka tarehe 10/08/24 tuone kama Elie Mpanzu atatangazwa kujiunga na Club yoyote hapa na most likely atajiunga Simba au Yanga sioni club nyingine ambayo atajiunga.

Nitaleta Post ingine ya Kulinganisha Uwezo wa Winga Kibu Denis, na Max Mpia Nzengeli.View attachment 3059197
Hakuna mchezaji anakwenda ulaya bahati mbaya mzinze akiwa bora utamuona anamfuata mpanzu ulaya.
 
Maxi Mpia Nzingeli
Ndio maana nikauliza kuna mawinga wangapi wa maana Yanga, umemtaja huyo winga mmoja pekee. Maxi alianza vizuri sana katika kutekeleza majukumu yote kwa ufanisi ila siku hizi amekuwa ni mzuri sana kwenye ukabaji zaidi ila kwenye ushambuliaji anafeli katika kufanya maamuzi sahihi ya mwisho. Atalazimisha kushuti wakat kuna mtu wa kumpenyezea nafasi, kutumia nafasi nako anayoipata imekuwa ni mtihani hatulii anapokuwa golini. Ila yote yote ni mtu anayejituma sana uwanjani na kupiga kazi haswa hasa kwenye ukabaji.
 
Back
Top Bottom