Rubi
JF-Expert Member
- Oct 5, 2009
- 1,615
- 331
Kuna mwalimu wangu (umri wake, sijui lakini ni mtu mzima kwenye miaka 50) ambaye amekuwa kama rafiki na kama mama yangu! ana tatizo linamsumbua la miguu kuuma. Miguu yenyewe inavyomuuma ni sehemu ya mbele kwenye ugoko lakini sio kwenye mifupa ni kwenye nyama eneo la kati.
Sehemu nyingine kama kwenye joint n.k hasikii maumivu yoyote hivyo anaweza kutembea , kuchuchumaa, kubeba vitu n.k. tatizo ni hilo eneo la kati kwenye miguu yote miwili anasema inawaka kama moto, usiku halali na ameshakwenda kwenye hosipitali mbalimbali na dawa mbalimbali ametumia. hata niandikapo hapa yuko anatumia dawa lakini anadai hakuna nafuu. na anasema hosipitali walimwambia watampiga e-ray mara baada ya kumaliza dawa ingawa wamemwambia kuwa wanamashaka kama wataona kitu kwa kuwa tatizo liko kwenye nyamasio kwenye mifupa.
Kwa kweli kama binadamu nimemuhurumia kwa mateso anayopata na kibaya zaidi anaonekana kukata tamaa mpaka kuhisi labda amerogwa. ingawa tunampa moyo asifikiri hivyo ila maumivu ayapatayo bila kujua ni nini ndio yanayompotezea tumaini.
Hivyo wa JF najua jukwaa hili ni zaidi ya shule mbali ya kuwa msaada kwa wengi pengine nami nitaweza kupata chochote kutoka kwenu nitakachoweza kumsaidia.