Kwa wale wote walionipongeza kwa kuwapa nasaha zangu kwenye hili jukwaa la J.F. Doctor nawapeeni zawadi yangu hii. Fanyeni hivi kila siku unapoamka asubuhi kabla ya kula kitu ukisha piga mswaki chemsha Maji ya Uvuguvugu glasi
moja tia kijiko kikubwa cha kulia wali Asali safi ya nyuki kwenye hiyo glasi ya maji ya uvuguvugu, unywe kila siku asubuhi
kabla ya kula kitu uwe unafanya hivyo katika maisha yako yote. Kisha uwe unakunywa Asali kijiko kimoja kila siku Asubuhi kabla ya kula kitu na usiku baada ya kula chakula kwa muda wa siku 40 hiyo inasaidia kusafisha ini na figo huo ndio usia
wangu Mkuu. kwani katika Mwili wa Binadamu kuna kila kiungo chake kina faida na umuhimu wake lakini viungo hivi Muhimu sana yaani Moyo,figo,Ini,nyongo, na Bandama ni viungo muhimu sana kwa binadamu kufanya kazi yake barabara itabidi tuwe waangalifu wa vyakula tunavyokula kwa ajili ya afya zetu asanteni sana.