Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imebadili uwanja na muda wa kuanza kwa mchezo namba 167 wa Ligi Kuu ya NBC baina ya Simba na Azam ambao ulipangwa kufanyika kwenye Uwanja wa KMC Complex, Februari 24,2025 kuanzia saa 10:00 ambapo sasa utafanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa siku hiyohiyo kuanzia saa 1:00 usiku.
Taarifa iliyotolewa na TPLB leo imesema kuwa sababu ya mabadiliko hayo ni kutoa fursa kwa mashabiki wengi kutazama.
"Sababu ya mabadiliko hayo ni kutoa nafasi kwa mashabiki wengi zaidi kuhudhuria mchezo huo ambao ni moja ya michezo mikubwa ya Ligi Kuu ya NBC inayovuta hisia za watu wengi.
"Uwanja wa Benjamin Mkapa wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 60,000 umekuwa ukitumika kwa michezo mingi mikubwa na inayohusisha mashabiki wengi zaidi."