Mzizima derby (Simba vs Azam) imepoteza mvuto

Mzizima derby (Simba vs Azam) imepoteza mvuto

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
9,091
Reaction score
21,087
Hii ilikuwa Moja ya derby kubwa hapa Tanzania baada ya Ile ya Simba. Vs Yanga

Ila Kwa Sasa ni kama mechi ya kawaida kabisa, watu hawana habari nayo
Bado siku 1 hii derby ipigwe lakini hakuna anayejali,
Watu wanaongelea mechi Mashujaa vs Yanga, hii imesikitisha sana

Inasemekana kitu kilichoouwa hii derby ni matukio ya kupanga matokeo,
Inasemekana Azam Huwa anawaachia Simba kufunga ili kama njia ya kufanya awe bingwa kirahisi ili urafiki wao udumu

Tukumbuke Azam alitoka wachezaji wake kwenda kuwasidia Simba kuwa bingwa
Erasto Nyoni
Paschal Wawa
Shomari Kapombe
Aishi Manula
John Boko
Pia inasemekana Azam watawazadia Simba wachezaji 2 hatari yaani Feitoto na Sillah msimu ujao

Wachezaji wa zamani wa Azam Amri kiemba na Dube waliweka wazi kuwa Azam fc- Huwa anafihia kufungwa na Simba na siku ya mechi ya Simba Azam Huwa hawajiandai kabisa

Tusishangae hiyo mechi hata uwanja wa Azam complex usikae, maana mashabiki tunajua kuwa Azam anaenda kumpa point mnyama wala hatajisumbua
 
Tuko busy tunajiandaa na CAF.....
Hyo derby mnailazimisha hakuna Derby hapo...
Na haijawahi kuwa mvuto labda mvuto mtauleta nyinyi mkishachapwa na Azam...
 
Tuko busy tunajiandaa na CAF.....
Hyo derby mnailazimisha hakuna Derby hapo...
Na haijawahi kuwa mvuto labda mvuto mtauleta nyinyi mkishachapwa na Azam...
Mna urafiki wa kudumu
 
"Tunataka kuona katika Taifa hili, vijana jeuri na wenye kujiamini, si vijana waoga, akina "ndiyo bwana mkubwa", vijana wanaohoji na kupiga vita mifumo ya jamii isiyoshabihiana na matakwa na matarajio ya jamii ya kitanzania. Tunataka vijana waasi dhidi ya mifumo kandamizi, ubwana na ufisadi katika Taifa"

Mwl J.K. Nyerere, Rais wa Kwanza wa Tanzania
 
Na kusapoti hoja ya mleta mada, oneni jinsi ambavyo Azam huwa inavyomsaidia Simba kwa kumpa pwenti 3 za bure kila wakikutana.

1000053013.jpg
 
Kichekesho utashangaa kwenye hiyo mechi anapangwa tena mwamuzi wa mchongo kama yule wa mechi na Namungo! Hii nchi kuna mambo yanastaajabisha sana.
 
Back
Top Bottom