"Mzoea vya kunyonga vya kuchinja Haviwezi". Hongera Halima Mdee na Makamanda wote kwa kugomea wito wa kienyejienyeji

Katika maisha ya mwanadamu, ipo imani kwamba kadri umri unavyozidi kwenda, na ndivyo hekima na busara kwa mwanadamu huyo inavyozidi kuongezeka. Imani hii kwako Pascha Mayala iko tofauti. Nakumbuka wewe ni mwandishi wa habari mbobezi hilo sina shaka nalo. Lakini andiko uliloandika umeandika kana kwamba wewe sio mwandishi wa habari mbobezi. uandishi wako wa bandiko hili hauna balance yoyote kwa sababu umeandika mlongo wa mambo lakini kwa kuangalia upande mmoja tu wa mashoga zako. Katika tamthilia yako ni wapi ambapo umeandika kuonyesha utaratibu wa kupeleka majina Tume ya uchaguzi kama ulifuatwa au ulikiukwa. Kama huna hoja za msingi kwa umri wako ni bora ukakaa kimya kulinda heshima yako.Vingenevyo tutakujibu tu. Eti hawakwenda mbona tumewaona wakishuka ndani ya Coaster. Watu waache ushabiki maandazi.Leta hoja na sio vioja
 
Mbona kama uwezo wako unakuwa mdogo sana ivi ni wewe kweli
 
Umebwabwaja weeee enzi za jk, hukupata uteuzi, enzi mwendazake msukuma mwenzio hukupata uteuzi, sasa kaja mama unapanua domo kila uchao sasa umerudi CHADEMA.
Baki huko ccm na utazeeka bila uteuzi nyau wewe.
Nilikuona great thinker kumbe poyoyo
Kiukweli huyu jamaa mbona amekuwa mjinga kiasi hiki duuu inasikitisha sana
 

unatetea huu uvunjifu wa sheria, halafu ajabu unawalaumu Chadema kila siku hawatendi haki, wakati walifuata sheria na taratibu zao kuwaadhibu wale wanawake, hueleweki bro.
Hapa Mkuu denooJ nakuomba sana be honest kwasababu hapa ndipo karma inapolalia, Chadema walifuata sheria na taratibu zao kuwaadhibu, naomba unielimishe walifuata vipi?. Ikikupendeza anzisha uzi wa jinsi Chadema inavyofuata katiba yake, sheria, taratibu na kanuni katika kuwaadhibu watovu mbalimbali wa nidhamu ndani ya chama.
Vinginevyo ukipata muda, pitia nyuzi hizi, humu ujibu Chadema ilifanyagaje
Anza na
Hapa Uamuzi wa CHADEMA dhidi ya madiwani: "A Big Mistake!"
Kisha hapa Wito: CHADEMA Watendeeni Haki Wanachama Wenu Ili Kuwatendea Haki Watanzania 2015!
Kisha Opinion: Kung'atuka Kwa Zitto, CHADEMA, Msishangilie, Mkajisahau, Jiandaeni kwa "Karma!"
Na sasa Mmezoea vya kunyonga hamviwezi vya kuchinja. Hongera sana Halima Mdee na Makamanda wote kwa kugomea wito wa kienyejienyeji

P
 
Kuelekea siku ya wanawake duniani, Halima Mdee anastahili pongezi za dhati, ni Mwanamke wa Shoka.
Update
Hatimaye Chadema wameacha kushupaza shingo na wamekubali matokeo!, kwa kuufuata ushauri wa bandiko hili CHADEMA kubalini matokeo na m-survive, or shupazeni shingo. You go to hell 6ft under Hao Makamanda 19 ni mashujaa, kuendelea Ubunge wao

Nimepokea taarifa, hii kutokea twitwani Kisha nikasoma na bandiko hili humu JF Tundu Lissu: CHADEMA tumeanza kupokea Ruzuku

Chadema wameufuata ushauri wa bandiko hili, waneacha ujinga wa kujifanya hawayatambui matokeo ya uchaguzi wa 2020!, sasa wameacha kushupaza shingo, wameyatambua matokeo kimya kimya!, wamewasamehe mashujaa hawa kimya kimya msamaha ambao utatangazwa rasmi siku ya Jumatano tarehe 8 Machi na Mwenyekiti wa Chadema, mbele ya Rais Samia!.

Iliwa kusemwa kuwa hakuna mkate mgumu wowote mbele ya chai!, tayari Chadema imeisha anza kupokea ruzuku hivyo sasa ita survive!. Na ile kesi ya kina Halima Mdee na wale 19 iliyopo mahakamani itafutwa!.

Hongera sana Chadema, for doing the right thing!, mtabarikiwa, viongozi wenu watabarikiwa, chama chenu kitabarikiwa na Tanzania Itabarikiwa!.
Mungu ibariki Chadema
Mungu ibariki CCM kwa kukubali reconciliation
Mungu ibariki Tanzania
Paskali
 
Hiyo taarifa ya twitter hata sijui kwanini umeiamini, very shallow.
 
Leo ndio siku yenyewe ya wanawake duniani, hongera sana kwa wanawake wote duniani akiwemo Mwanamke huyu!.
P
 
Nimeisoma hukumu, kwenye hili, Chadema haina jinsi, lazima ijifunze kuchinja, sio kila siku kunyonga tuu!.

1. Mahakama zetu zinarudia makosa yale yale ya ukosefu wa kutenda haki kwa sababu ya legal technicalities, kuwa Mahakama haiwezi kutoa uamuzi wa kitu ambacho hakikuombwa!.
2. Wabunge hawa 19 wa Chadema, walivuliwa uanachama wao kinyume cha katiba ya JMT na kinyume cha haki kwa kutokusikilizwa, kinyume cha katiba ya Chadema kwa kukiuka sheria, taratibu na kanuni!.
3. Kikao cha CCM ya Chadema, kilichowatimua kilikaa kama a kangaroo court na kutoa maamuzi ya kikangaroo!.
4. Katiba ya Chadema inasema mwanachama kabla hajafutwa uanachama, kwanza atatumiwa hati ya mashitaka kwa maandishi by despatch, kisha atapewa siku 14 za kujibu mashitaka. Chadema hawakuandaa hati zozote za mashitaka!. Hili Mahakama ilipaswa ilione!.
5. Baada ya watuhumiwa kupewa hati ya mashitaka, ndipo kikao cha CC kinaitishwa kama mamlaka ya nidhamu, kusoma majibu ya mashitaka, na ndipo kinawaita washikiwa na kuwasikiliza. Hili halikufanyika!.
6. Baada ya wabunge 19 wa Chadema kuapishwa, hapa Chadema waliposwa kufanya kitu kinachoitwa a due process ya nidhamu na sio zile Zimamoto za kikangaroo!. There was no emergency of whatsoever!. Mahakama ilipaswa ilione hili!.
7. Uthibitisho wa hakukuwa na any emergency ya kuitisha CC, ni the time taken, kuitisha kikao cha Baraza Kuu!.
8. Baada ya kuitishwa kikao cha Baraza Kuu, kitu cha kwanza kwa Baraza Kuu Chadema kuangalia ni uhalali wa kikao cha CC, pili jee katiba, sheria, taratibu na kanuni za mamlaka ya nidhamu ya Chadema zilifuatwa?.
8. CC ya Chadema ni mamlaka halali ya nidhamu ya wabunge wa Chadema, lakini CC ya Chadema sio mamlaka ya nidhamu ya Halima Mdee ambaye ni Mwenyekiti wa Bawacha!, Mamlaka yake ya nidhamu ni Baraza Kuu!, CC ya Chadema ilipata wapi mamlaka ya kumtimua Halima Mdee?!. Kikao cha Baraza Kuu kilipaswa hili kukuona!.
9. Japo kikao cha Baraza Kuu Chadema kiliitishwa kihalali kama mamlaka ya rufaa ya wabunge wa Chadema, lakini kitendo cha kikao hicho kubariki uamuzi wa CC kuwatimua bila kufanya mapitio yoyote, ni uthibitisho wa Chadema bado ni chama kichanga, mfano kingechukua nchi ile 2015!, it would have been disastrous!.
10. Kitendo cha Baraza Kuu kubariki maamuzi ya kikangaroo ya CC ya Chadema, kilifanya niyaite maamuzi yale pia ni ya kikangaroo, na kitendo cha Mahakama Kuu kuyabari maamuzi ya kikangaroo, Mahakama Kuu yetu nayo has joined the team!.
A Way Forward
1. Kwa vile Chadema imefanikiwa kuwatimua hao 19 sasa Chadema isikate tena rufaa, kupinga uamuzi huu, bali iitishe kikao cha Baraza Kuu , ASAP, kifanye a due process, hili la wabunge 19 liishe, wabunge hao 19 wavuliwe ubunge wao, Chadema wapeleke majina 19 mengine, wateuliwe waapishwe, tuwe na Bunge la vyama vingi!.

2. Chadema wakifanya tuu dillydalling kukaa rufaa, inakula kwao!. By the time rufaa inasikilizwa, ndipo kifuate kikao cha Baraza Kuu, I'm afraid the time left before the next election is too little too late, ikibaki muda wa chini ya miezi 12 kabla ya muda wa uhai wa Bunge kuisha, hakuna uchaguzi wowote wala uteuzi wowote wa wabunge wapya!.
3. Tena nashauri kikao hicho cha Baraza Kuu, pia sasa ndio kimtimue Halima Mdee, kikifuatiwa Mkutano Mkuu kuthibitisha. Hapa najua changamoto ni fedha!, kule kwenye kile chungu, zilikopatikana zile fedha za kugharimia Baraza Kuu lile, kile chungu bado kipo, kitagharimia vikao vyote viwili, na Chadema inaweza kupiga ndege wawili kwa jiwe moja kwa mtu kupumzishwa kwa heshima na dereva mpya kupatikana!.
Paskali.
 

Sasa hizi mkuu za wanachama kufukuzwa bunge likadinda na longo longo zote za technicalities ni kwa chadema tu?

Tumeyaona na kina shilinde, lijua lipole nk, lakini siyo na kina Sophie Chui!
 
Hivi Paskali kujipendekeza kwa serikali ya ccm kutaisha lini na umri unazidi kukutupa mkono ?, sasa hivi ulitakiwa ufikie mahala unafikiria kwanza kabla ya kuandika jambo, umri wako unapingana na mambo unayoyafanya..
Sasa hivi umekuwa zaidi ya kiherehere yaani sio zoba sio zombie sijui nikuita jina gani hasa
 
Mwite Paskali Chongolo...huenda akakumbuka kitu kuhusu CCM....

Katibu wa CCM aliyetoswa Ndg Chongolo ametoa Somo kubwa...Wacha aendelee kujipendekeza tu.

Sent from my M10_Max using JamiiForums mobile app
 
Kiukweli kabisa humu JF tuna mijitu mijinga ajabu!. Ni mjinga tuu asiye na uwezo wa kuchambua hoja za kisheria ndie atafikiri mimi najipendekeza, in my life sijawahi kujipendekeza kwa yeyote na kwa lolote!.
Japo mimi ni kada wa CCM, lakini mimi sio kada chawa, ndio maana naweza kukiambia chama changu hoja kama hizi
View: https://youtu.be/Qr6j25jFGyI?feature=shared
Mtu anayejipendeleza CCM anaweza kushauri hivi
Na kama ulidhani najipendekeza kwa JPM, mtu anayejipendekeza anaweza kuuliza swali kama hili
View: https://youtu.be/Ta0URHvUlko?si=KzEGTkgzj51gyIWS au mtu wa kujipendekeza anaweza kutoa hoja kama hii in public?
View: https://youtu.be/A_YPEHtM9WM?si=mXdk1TpIfeEqo0I4 Hebu acheni huu ujinga!.

P
 
Wewe zoba tu paskali hata useme nini, nilikuwa nakuona bonge la mtu wakati ule, lakini mara baada ya kujitoa akili na kubeba akili za kushikiwa za ccm umekuwa zoba wa kiwango cha juu saana
 
Wewe zoba tu paskali hata useme nini, nilikuwa nakuona bonge la mtu wakati ule, lakini mara baada ya kujitoa akili na kubeba akili za kushikiwa za ccm umekuwa zoba wa kiwango cha juu saana
Na ninatamani ungejitambua ukayaona unayoandika kwa sasa ni upuuzi ukaamua kuyaacha ungerudisha heshima yako kwa haraka sana, kila mtu huwa anakengeuka, unakumbuka siku ile magufuri alikukejeri ulipouliza swali ambalo lilionekana kwake la kipuuzi, na ni kwa sababu uliliuliza ovyovyo
 
Kitendo chako cha kuniita mimi mjinga unazidi kujivunjia heshima wewe binafsi, na utadharauliwa na kila mtu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…