Mzumbe: Je hawa Wahadhiri wafukuzwe kazi?

Mzumbe: Je hawa Wahadhiri wafukuzwe kazi?

MzalendoHalisi

JF-Expert Member
Joined
Jun 24, 2007
Posts
4,679
Reaction score
1,612
Mzumbe dons in PhD scam

Eight senior lecturers with the Mzumbe University have doctorate degrees that are either fake or acquired from institutions that lack internationally accepted accreditation, the Tanzania Commission of Universities (TCU) said today. TCU Executive

Source: Daily News 11/02

Wandugu- Je hawa wahadhiri wafanyweje? Washushwe vyeo au wafukuzwe kazi kwa kudanganya?????????

Sheria ya Elimu ya Juu inasemaje?
 
Tatizo uwaajiri au upandishaji vyeo bila ya uhakiki wa mdhubuti. Wacha waummbuane Vyuo Vikuu .. Wahakiki pia Baraza la mawaziri, Bunge, na dara za serikalini.
 
Ukisoma kwa makini hiyo taarifa ya Nkunya utagundua kuwa yeye mwenyewe hajui ni hatua gani za kuwachukulia hao madaktari wa Mzumbe. Hoja yake ni kuwa TCU haina meno kisheria.

Lakini labda tuseme hao jamaa ni miongoni mwa watanzania wengi (wakiwemo hata viongozi wa serikali) ambao wamekuwa victims of scam. Pengine ni jamaa wazuri tu wenye nia ya kujiendeleza kielimu. Halafu na hizi nadharia za kisasa za kusema elimu si lazima ipatikane kwenye vyumba vya kuta nne, zinachangia sana kuwachanganya watu ambao wako desperate kupata vyeti.

Ushauri wangu ni kuwa hivyo vyeti vyao visitambulike, ila hakuna sababu za msingi za kisheria kuwafungulia mashtaka. Ni kwamba wamejiendeleza lakini kiwango walichosomea hakilingani na vyeti walivyopata. Na mtanzania yeyote anayo haki ya kujiendeleza mpaka upeo wa uwezo wake, ama sivyo?
 
Ukweli utabaki palepale, kugushi, kutapeli, plagiarism, etc ni makosa yaliyo na sheria za kushughurika na watendaji wamambo haya. Pamoja kuwa TCU haina meno nivema serikari ikaamua kuwapa meno TCU lakini hawa wahusika washughurikiwe kama fundisho na wakishashughurikiwa kama wanabasic qualification kufundisha university basi warudishe chuoni kama tutorial assistants.
 
Hivi sheria za nchi yetu tukufu ya Tanzania zinatoa adhabu gani kwa mtu aliyefoji vyeti na kupata madaraka muhimu katika jamii ya watanzania, kama hawa wahadhiri wa Chuo Kikuu cha MZUMBE, au yule mbunge wa CCM Chitalilo anayesemekana alitumia vyeti feki vilivyomwezesha kuwadanganya wapiga kura na kupata ubunge na halafu bunge kutumchukua hatua zozote baada kuthibitishwa na polisi kwamba vyeti vyake ni feki!!!!!!!???????.
 
Mods,

Hii yaweza kuunganishwa na ile thread nyingine "Mzumbe dons in PhD scam" ili tupata mabandiko ya kipamoja

Ahsanteni
 
Back
Top Bottom