Ukisoma kwa makini hiyo taarifa ya Nkunya utagundua kuwa yeye mwenyewe hajui ni hatua gani za kuwachukulia hao madaktari wa Mzumbe. Hoja yake ni kuwa TCU haina meno kisheria.
Lakini labda tuseme hao jamaa ni miongoni mwa watanzania wengi (wakiwemo hata viongozi wa serikali) ambao wamekuwa victims of scam. Pengine ni jamaa wazuri tu wenye nia ya kujiendeleza kielimu. Halafu na hizi nadharia za kisasa za kusema elimu si lazima ipatikane kwenye vyumba vya kuta nne, zinachangia sana kuwachanganya watu ambao wako desperate kupata vyeti.
Ushauri wangu ni kuwa hivyo vyeti vyao visitambulike, ila hakuna sababu za msingi za kisheria kuwafungulia mashtaka. Ni kwamba wamejiendeleza lakini kiwango walichosomea hakilingani na vyeti walivyopata. Na mtanzania yeyote anayo haki ya kujiendeleza mpaka upeo wa uwezo wake, ama sivyo?