Mzungu anaetalii kwa baiskeli aanza safari Uvinza - Mpanda, kalala porini usiku, aombwa pampu kujaza tairi la gari, Nyoka aingia kwenye hema

Mzungu anaetalii kwa baiskeli aanza safari Uvinza - Mpanda, kalala porini usiku, aombwa pampu kujaza tairi la gari, Nyoka aingia kwenye hema

gearbox

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2024
Posts
563
Reaction score
1,768
Kino Yves, Ni mfaransa anaezunguka nchi mbali mbali na baiskeli yake ya kulala, Katalii nchi nyingi Afrika kama Misri, Sudan, Ethiopia, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na sasa yupo Tanzania.

Ni katika muendeleo wa Utalii wake akituonyesha video zake, Baada ya Kigoma - Uvinza kwa sasa kaanza safari nyingine ya Uvinza - Mpandakilometa 200, Ni safari ndefu kaikadiria kutumia siku tatu, kwa siku ya kwanza kapiga peda kilometa 60

Safari kwa baiskeli imekuwa shughuli pevu kwake, barabara ya Uvinza - Mpanda ni ya vumbi na kwa mvua zinazoendelea kuna baadhi ya sehemu kuwa tope, Mazingira ya narabara ni porini

Porini hakuna miji hivyo imebidi alale kwenye hema usiku mzima

Kwenye hema kamkuta nyoka, katika harakati za kumtoa yupo mashakaani kama nyoka kamngata au lah !

Video imewekwa kwa ubora mdogo kuzingatia matumizi kidogo ya bando

 
Kulala porini usiku kwenye hicho kihema chake inahitaji uwe ngangari
 
Duuuh nawaza tu usalama wakora wasije wakampiga panga
 
Duu Sasa kama ameng'atwa itakuaje maana yeye mwenyewe hana uhakika
 
Binafsi my dream ni kuizunguka Tanzania mikoa yote nikanyage na mguu wangu ila nitakuwa na private car
 
Back
Top Bottom