Mzungu Kichaa amponda Ali Kiba na kufunguka juu ya malipo ya mamilioni ya pesa huko Ujerumani

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
Lakini kumekuwepo baadhi ya wasanii ambao wakati mwingine hutengeneza mazingira ya uongo hasa kupitia mitandao ya kijamii, na wengine hata kufanya na Interviews ili tu kufanya watu waamini kuwa thamani yao pia iko juu.

Mzungu Kichaa yuko tofauti kidogo katika hilo, sababu haoni sababu ya msanii kudanganya kwa kitu ambacho sio kweli. Msanii huyo wa Denmark aliyeishi Tanzania kwa miaka mingi alizunguzungumzia swala hilo katika kipindi cha Sporah.

“Mimi siwezi kwenda kwenye vyombo vya habari na kusema ooh nimetengeneza milioni 100 kwenye show halafu media zote ziseme ‘oooh wow’…kama alivyofanya Alikiba kipindi fulani” Alisema Mzungu Kichaa. “Alisema alikuwa anataka kwenda kufanya show Ujerumani, na alikuja kusema ameahirisha kwenda, tena aliahirisha siku moja kabla, na kusema kuwa angelipwa shilingi milioni 100…Kwahiyo akadai kwamba alikuwa anapewa hiyo hela lakini mikataba haikwenda kama ilivyotakiwa so aliahirisha show siku moja kabla, na kama mwanamuziki mimi najua jinsi mambo ambavyo hua yanakuwa, siamini watu waliokuwa tayari kumlipa kiasi cha pesa kama hicho…na kwa wao kutafuta media publicity kupretend we are getting big money to perform nadhani hilo ni kosa.” Alimaliza.
 
Huyu nae kachoka tu si aende huko akajichanganye na kina Chriss Brown
Ally Kiba hata wasemejee dogo anaimbaa balaa na nyimbo zake hazichosh kusikilizaaa apelekee ukichaa wake Holwoody tumuonee
 
Huyu nae kachoka tu si aende huko akajichanganye na kina Chriss Brown
Ally Kiba hata wasemejee dogo anaimbaa balaa na nyimbo zake hazichosh kusikilizaaa apelekee ukichaa wake Holwoody tumuonee

Uyo mzungu kichaa hajachoka ila hapendi wasanii waonyeshe na kujisifia mali zao wakati mashabiki zao wengi masikini.

Pia kuhusu swala la ali kiba mzungu kichaa hapendi wasanii wa wanalipwa kidogo show za nje harafu wanadanganya kwenye mitandao kuwa wamelipwa pesa ndefu.

Pia rushwa kwa madj ili wapige nyimbo zako hapendi sana ili jambo na yeye hukataa kutoa rushwa.

Ili lilipelekea kufukuzwa kwenye kituo kimoja cha redio alipopeleka kazi yake.

Pamoja na kwamba hapa Tz hafanyi sana show lakin anapata show nyingi kenya, uganda, ulaya etc.

Uyo mzungu kichaa niliwai kukutana naye London akaniambia mambo mengi yanayoendelea kwenye music tz kuna mengine yanasikitisha.

Kwa ufupi mzungu kichaa yuko poa sana na ilo jina mzungu kichaa alipewa na juma nature.

Yeye alikuwa hapendi aitwe mzungu. Juma nature akampa jina la mzungu kichaa kutokana na mzungu huyo kujimix sana. Alimpa ilo jina wakiwa studio.

Nina habari nyingi kumuhusu ngoja niishie hapa
 
Kaongea ukweli bana kwa mtonyo upi wa kuacha millioni 100 kibongobongo angekuwa level hizo angeenda kukopa ili ajenge...

Ndo yaleyale aliyosemaga Dudubaya enzi zile Mr. Nice anahit kufanya show nje, Duduakasema hawa wengi wanaenda kutumbuiza ubatizo, kipaimara na birthday alafu wanadai wanashow nje... bongo bana ulimbukeni mwingi.
 

Hiyo redio na hisi clouds maana jamaa wanapendwa kunyenyekewa utadhani maboss vile.
 
Hakutaja redio ila mi siwezi jua ni ipi maana redio zote ni wale wale madj ndio mameneja

Yah ni mara nyingi inakuwa hivyo. Nakumbuka Ailer alipokuwa anahojiwa clouds jamaa alimuuliza una meneja,akasema bado. Jamaa akamweleza sio tatizo utapata hapa hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…