Mzunguko wa dunia katika mhimili wake

Daby

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2014
Posts
33,894
Reaction score
76,810
Wakuu ninaswali kama sio maswali.
Ni hivi dunia inajizungusha kwenye mhimili wake tunapata usiku na mchana hapo sawa.

Sasa ishu inakuja kwanini hatushuhuudii/kuhisi mzunguko huo? Je ni kwasababu nilipo au ulipo ni sehemu ndogo ya huo mzunguko ndiyo maana siuhisi au kuuona huo mzunguko?

Kama jibu ni ndiyo..je ndege ikiwa angani kwanini abiria usione jinsi dunia inavyozunguka kwa maana ndege inakuwa imeshatoka duniani? Kama sio kuona kutokana na speed ni kubwa saana kwanini hata usihisi? Je ndege inatumia technolojia gani kukimbiza/kufukuzia sehemu ya dunia inapoenda kutua maana itakuwa inazunguka AKA INAHAMA KWA SPEED KUBWA? Hayo yote yakitegemea speed ya mzunguko wa dunia ni 40000 ÷24 = 1670km/hour. Gari lenyewe speed 100 au 120 ni unatoa machozi kama unachungulia nje.

Ndege inawezaje kufukuzia hiyo speed? Na wakati normal speed ya ndege ni 475 km/hour to 540km/hour?
(nipo tayari kurekebishwa)

Majibu ya maswali haya yatakuwa mwendelezo wa maswali mengine.
 

Huhisi mzunguko huu kwa sababu kila kitu kwenye uso wa dunia, pamoja na atmosphere, vinazunguka kwa mwendo huu.

Chukulia mfano wa sisimizi aliye katika gari linaloenda kasi. Sisimizi anakuwa na "kinetic energy" ya gari, na kama gari linaenda 90 km/hr, madirisha yamefungwa, hata hewa iliyo katika gari inakwenda kwa speed hiyo na sisimizi anakuwa hajui kwamba gari lina mwendo

Sasa wewe na dunia unakuwa mdogo mara nyingi sana zaidi ya sisimizi alivyo ndogo kwa gari.

Kama jibu ni ndiyo..je ndege ikiwa angani kwanini abiria usione jinsi dunia inavyozunguka kwa maana ndege inakuwa imeshatoka duniani?

Ndege haijatoka duniani bado, ipo katika atmosphere inayozunguka na mwendo wa dunia. Mfano mzuri wa kuona dunia inavyozunguka ni kwenda kwenye satellite zilizotoka nje ya atmpsphere ya dunia na zinazoweza kuiona dunia kwa mbali. Mfano ni "International Space Station"


Swali lina assume ndege imetoka nje ya dunia. Tumeona hapo juu kwamba hewa ya dunia ni sehemu ya dunia na ndege haitoki nje ya dunia.

Ndege inawezaje kufukuzia hiyo speed? Na wakati normal speed ya ndege ni 475 km/hour to 540km/hour?
(nipo tayari kurekebishwa)

Again, ndege yenyewe ipo katika dunia na inasukumwa na speed ya dunia. Ni sawa na wewe ukae nyuma kwenye pickup, halafu pickup iwe inaenda kasi, halafu uchukue kitenesi na kukirusha juu kidogo halafu ujaribu kukidaka. Unaweza kufikiri kwamba kitenesi kitadondoka nje, lakini kama hakuna upepo na hujakirusha juu sana utaweza kukidaka kama mtu ambaye kasimama, kwa sababu wewe, gari na kitenesi wote mna kinetic energy.

Ndege haitoki nje ya dunia, hivyo ni sehemu ya vyote vinavyokuwa moved na dunia vilivyo ndani ya dunia.

Nimejibu kutoka kichwani tu sijaangalia reference book kama nimekosea tujadili.
 
Ungekuwa mwalimu, ningepata A enzi zile,
 
Mwenzio kauliza, wewe badala ya kumjibu unatupa za kwako. Mtoto akishalala basi njoo na majibu sawa?
 
Wewe jamaa upo vizuri hope unafundisha twisheni some where. Big up sana
 
Acha story mingi
Weka musiki
 
Ni mechanism gani inayofanya dunia ijizungushe? Kama ni nguvu ya uvutani kwanini mzunguko uwe kutokaashariiki kuelekea magharibi
Na wewe umeongeza swali eeeeh
 

Haki ya nani una mbwembwe, LETA CHETI hapa yasijetokea ya BASHITE!!!!!!!
 
Mkubwa umetisha kwenye suala zima la "kujimegea"...
Tunasubiri nondo sasa tuelimike.
 
Huhisi mzunguko huu kwa sababu kila kitu kwenye uso wa dunia, pamoja na atmosphere, vinazunguka kwa mwendo huu.


Kwanza nishukuru kwa majibu murua..
Twende mbele..Kwanza mkuu mass ya dunia kupitia centrifugal force ndiyo vinafanya dunia kuzunguka kwa speed ambapo vitu vyote vinavutwa katikati? Right?
Sasa kama ni ndiyo je mass iliyopo kwenye atmosphere (maana huko kuna gases na tinny materials) ni sawa na iliyopo kwenye body la dunia hii hii? Kama sio kwanini speed isitofautiane. Na ni kitu gani kinafanya vitu viwili vikubwa vyenye uzito usioendana kuzunguka pamoja kwa speed ile ile?


Troposphere ni kweli inazunguka speed ile ile na Exosphere iliyopo karibu na jua. Na wanasema Exosphere is the layer where all molecules and atoms escape into the space. Escape escape wakati dunia all things are pulled into the center. Bado nina doubt na atmosphere kuzunguka pamoja na hili limviringo letu mkuu.
Hivyo hivyo kwa layers zingine naomba ufafanuzi mkuu

Stratosphere
Mesosphere
Thermosphere
Exosphere

????????????
 
Tukutane kwenye kutongoza wewe hapa unapwaya ndugu yangu
 
swali la kujiuliza:
TEKNOLOJIA SASAHIVI IMEKUWA, KILA SIKU NASA PAMOJA NA MASHIRIKA MENGINE YANATUMA ROCKET KWENDA ANGA ZA MBALI,
SASA TUSEME WAMESHINDWA KUTUMA CHOMBO CHA KURECORD DUNIA IKIZUNGUKA?
Bila ushahidi wa video mimi hawanipati
 
Aisee Mkuu maswali yako ni poa sana kwa kweli Mimi nilikuwa hobbyist mkubwa kabisa wa Astronomy na cosmologist nitakujibu kwa uelewa wangu and i stand to be corrected, Mimi nijuavyo Dunia Iko katika speed fulani ila vilivyopo ndani havihisi hiyo speed kwa sababu tu Havioni vitu vya nje ya Kufananisha navyo Na pia dunia iko katika constant velocity (Uniform velocity) Speed huonekana au kutambulika na Observers ikiwa tu kuna stationary object au kitu kingine ambacho hakiko ktk exactly same speed Mfano wewe upo katika gari ambayo ina tembea Kwa speed ya 120Km/H na mwenzio yupo katika gari ambayo ipo sawa speed na wewe regardless of stationary thing kama miti tu assume haipo basi ww toka dirishani umtaze mwenzio katika gari ingine ambayo uko Nayo same exactly speed basi mkitazamana japo upo katika mwendo mkali bado mtajiona stationary tu yani mtaona kama mmesima the same applied dunia tunaiona iko stationary na hatu feel hii speed of rotation kwa vile tu Tuna move nayo na hakuna vitu vya kujifanisha navyo amvayo viko stationary , Kaa kwenye gari funga vioo usiangalie nje gari itembee katika Speed constant ni wazi tu utahisi umesimama, mabadiliko ya speed na Kuona vitu vilivosimama hukufanya kugundua uko katika motion, secondary hakuna Aeroplane zinazotoka out of space zipo Rocket tu ambazo huenda angaa za mbali na zenyewe hutegemea Orbit zitakapo kuwa kuna kitu kinaitwa Parking orbit ukifika apo utaona dunia haitembeiii, Nikupe homework kama Dunia Inazunguka kwanini madishi ya Tv tunayaelekezea sehemu moja ili kunasa sattelite fulani kwanini hatuyazungushi kila muda?
 
swali la kujiuliza:
TEKNOLOJIA SASAHIVI IMEKUWA, KILA SIKU NASA PAMOJA NA MASHIRIKA MENGINE YANATUMA ROCKET KWENDA ANGA ZA MBALI,
SASA TUSEME WAMESHINDWA KUTUMA CHOMBO CHA KURECORD DUNIA IKIZUNGUKA?
Bila ushahidi wa video mimi hawanipati
Ingia youtube kuna video moja niliiona nikacheka kinoma...wanaonyesha jinsi inavyozunguka na sauti yake ..nahisi ile waliitengeneza kwenye The 100.

Ngoja niitafute niweke
 
Ah mabwege wale, video ya kutengeneza kabisa ile, wakawaweka jisauti bayabaya kama gurudumu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…