Mzunguko wa dunia katika mhimili wake

Uko sahihi dunia inazunguka pamoja na atmosphere yake...ndo maana eneo moja mvua inayesha hata masaa 24!!
 
Mkuu nimeanza kukuelewa.
Ni Kama upo kwenye ndege au gari ukimiminiwa juice au maji hayawezi kumwagika kwasababu wewe anayekuwekea..Maji na glass wote mpo katika speed moja. Hadi hapo sawa.

Kama mdau alivyosema atmosphere na earth zinaspeed tofauti kutokana na ingredients tofauti ndani yao je unaliongele aje hil? Speed ni moja au tofauti? Kama ni moja kwanini iwe hivyo na wakati ingredients ni tofauti?
 
Uko sahihi dunia inazunguka pamoja na atmosphere yake...ndo maana eneo moja mvua inayesha hata masaa 24!!
Hili haliwezi kuthibitisha kwasababu kuna mvua zinanyesha kwa kuhama/kutembea. Unaweza kushangaaa mvua ipo mombasa mara muda huo huo imehamia chanika.

Fikiria pia kuhusu speed ya mvua.

Usicheke ni njia ya kujifunza.
 
Km dunia inatembea pamoja na atmosphere yake inakuaje tunaona mawingu yanamove in different directions in different time
2. Tunasema dunia inajizungusha kwenye mhimili wake (earth's axis). Hii inamaana kunapoint fulani ya dunia ni north &south hazizunguki....swali langu ni kutaka kujua physically hizo point ziko sehemu gani kwenye uso wa dunia?
 
Brave quest. Je ni kweli speed ya mawingu ndiyo kali kuliko hii ya dunia? itabidi hii point yako niongezee nyama huko mwanzoni mkuu.

Ukianglia unaona mawingu yanakimbia saana. Sitaki kuamini kama huo ni upepo unaoonekana.
 
Sina tofauti kubwa na mdau, sababu hakuna official concept iliochukuliwa kati ya izo mbili mpaka sasa, bado ni study inayofanyiwa uchunguzi.

Tunaweza kusema hakuna speed sawa kwa ushahidi tunaouona kwenye Ionospheric motion kwamba charged particles zilizojuu zaidi angani hazi shei mwendo sawa na neutral particles zilizo kwenye atmosphere ya chini.

na pia tunaweza sema kuna speed sawa kwa sababu kuna imani kwenye research zilizofanyika kuwa, umbali wa kufikia 500km kutoka ardhini speed iko sawa kutokana na viscocity effect pamoja na charged particles again,

Kwaio utaona kuna mchanganyiko tofauti tofauti kwenye atmosphere unaosababisha mwendo sawa au tofauti lakini kwa sababu tofaut ni negligible basi utofauti uo uwa unaondolewa na pressure gradients.
 
Poa poa mkuu....
 
Swali rahisi sana izo point ziko north pole and south pole. kwa mfano upepo uko unaweza kua almost at stand still ila unaposogea kuelekea equator speed yake ndo inapozid kuwa kubwa
 
Dunia haizunguki, bali jua ndilo huzunguka ... Uthibitisho ni pale nabii Fulani aliposimamisha jua ili apigane na maadui..
 
Swali rahisi sana izo point ziko north pole and south pole. kwa mfano upepo uko unaweza kua almost at stand still ila unaposogea kuelekea equator speed yake ndo inapozid kuwa kubwa
[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
Dunia haizunguki, bali jua ndilo huzunguka ... Uthibitisho ni pale nabii Fulani aliposimamisha jua ili apigane na maadui..
 
Dunia haizunguki, bali jua ndilo huzunguka ... Uthibitisho ni pale nabii Fulani aliposimamisha jua ili apigane na maadui..
hehehe ulikuwepo kumshuhudia huyo nabii au na wewe uliambiwa ukameza?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…