Mzunguko wa pili ligi kuu tanzania kazi ipo ndani ya mkwakwani simba sc vs coastal union.

Mzunguko wa pili ligi kuu tanzania kazi ipo ndani ya mkwakwani simba sc vs coastal union.

Jospina

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2013
Posts
2,421
Reaction score
1,395
MZUNGUKO WA PILI LIGI KUU TANZANIA KAZI IPO NDANI YA MKWAKWANI SIMBA SC VS COASTAL UNION.
Wakati Simba SC imecheza mechi 12 huku ikishinda mechi 3 , droo 7 na kufungwa mechi 2 ipo nafasi ya 8 katika msimamo wa ligi na pointi 16 kibindoni wapinzani wao Coastal Union wao wamecheza mechi 13 huku wakishinda mechi 4 , droo 5 na kufungwa mechi 4 wapo nafasi ya 7 na pointi 17 .
Ukitazama uwiano kiufundi timu zote zinaonekana kushabihana.
Simba kadroo mechi 7 katika mechi 12 huku Coastal kadroo mechi 5 katika mechi 13, sasa 12-7= 5 wakati 13-5= 8 hapo utaona hakuna tofauti kabisa kwa sababu aliyecheza mechi nyingi ambaye ni coasta l anabebwa na droo ya mechi 5 huku Simba aliyecheza mechi chache anadroo 7 huku akishinda mechi 3 tu! Hapo utaona wote timu zao zinajilinda sana kuliko kushambulia ndio maana wana droo nyingi kuliko ushindi. Coastal kashinda mechi 4 Simba hiyo ndio inawapa tofauti ya pointi 1.
Timu zote zinategemea zaidi viungo wa kati na full backs kuanzisha mashambulizi hivyo utaona mpira mwingi unapigwa kati huku mashambulizi yakiwa ya kushitukiza au kutafuta zaidi ushindi kwa dead balls. Naweza sema Simba SC watakuwa na mtihani kidogo , sidhani kama backline ya Coastal itakubali kupoteza mechi 2 mfululizo. Game ya mwisho Wamefungwa 1-0 na YANGA.
DAKIKA 90 ZITAAMUA
 
Back
Top Bottom