asante sana kwa msaada wako nimeplan mwez huu wa tisa nitafata ulichonielekeza then ntakuja kukupa feedback asante mungu akubariki huendelee kutupatia hiyo elimu
Ubarikiwe pia ila kuna elimu ambayo nadhani unahitaji kuijua na hushauriwa kwa mwanamke anayetaraji kushika ujauzito.
Hakikisha kuwa kabla ya yote unakwenda hospitali na kufanyiwa vipimo ili kujua kama afya yako iko salama au la kwa ajili ya kushika mimba.
Vifuatavyo ni baadhi ya vipimo vinavyoshauriwa kufanywa:
1. General examination au uchunguzi wa jumla.
2. Kipimo cha kensa au Pap smear.
3. Kipimo cha magonjwa ya zinaa (STD) kama vile Chlamydia ambayo huweza kuathiri uwezo wako wa kushika mimba.
4. Kipimo cha damu cha kuangalia kama una upungufu wa damu, Rh na kinga yako ya mwili dhidi ya ugonjwa wa Rubella.
5. Kipimo cha mkojo cha kuchunguza iwapo una ugonjwa wa kisukari.
Ugonjwa wa kisukari huweza kumzuia mtu asishike mimba hata iwapo mzunguko wake wa mwezi uko sawa, anapata Ovulation na kidhahiri anaonekana hana tatizo lolote.
6. Kama una paka nyumbani au unakula sana nyama (red meat) pengine si vibaya pia kupima kipimo cha Toxopmasmosis infection.
7. Kuyajua na kuzingatia baadhi ya mambo yanayoathiri kushika mimba ambayo ni pamoja na:-
• Ingawa unene unaweza kumzuia mtu asishike mimba lakini kufanya mazoezi sana na kuwa na uzito mdogo sana wa zaidi ya kilo 50 huweza pia kumsababisha mtu asishike mimba. Mazoezi ya kupindukia pia huathiri homoni mwiilini.
• Kuwa na fikra nyingi na msongo wa mawazo 'stress' huweza pia kauthairi uwezo wa mtu wa kushika mimba.
• Kutokula vizuri na kutopenda kula kwani humkosesha mwanamke au hata mwanamme baadhi ya virutubisho muhimu vinavyotakiwa kwa ajili ya kufanikisha suala la kushika mimba.
• Sigara, marijuana na pombe ni miongoni mwa vitu ambavyo vinaweza kuathiri uwezo wa kubeba mimba.
Na mengineyo mengi ambayo ukifika hospitali utashauriwa ikiwemo na matumizi ya virutubisho kadha wa kadha kama matumizi ya vidonge vya Folic