Mzungumzaji mhamasishaji/ motivational speaker

Mzungumzaji mhamasishaji/ motivational speaker

Ngwananzengo

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2012
Posts
1,911
Reaction score
1,315
Mimi ni MZUNGUMZAJI MHAMASISHAJI, pengine kwa utangulizi nieleze nini maana hasa ya MM. MM ni mtu anaezungumza ktk hadhira akiwa na lengo mahsusi la kupandikiza mbegu za uthubutu na kujitambua kwa hadhira. Hadhira yaweza kuwa wafanyakazi wa kampuni, kikundi cha uzalishaji Mali, wafanyabiashara au watu mchanganyiko wenye lengo na dhamira ya kuongeza tija na ufanisi ktk shughuli zao.
Kwa mtu anaependa kuelewa zaidi au kunihitaji aniPM. Pia kwa wenye kujua au kupenda kuongezea jambo karibuni. Mimi nipo tayari kutoa huduma hii popote pale. KARIBUNI.
 
Tuwekee video zako za youtube tupate uhakika vizuri...
 
Tuwekee video zako za youtube tupate uhakika vizuri...
Au sijakuelewa vzr? Maana hoja yako imejikita ktk wasiwasi ulionao juu yangu na si katika kufahamu kazi zangu. Maana inavyoonekana unataka video ili uone kama kweli mimi ni MZUNGUMZAJI MHAMASISHAJI na si kuona video ili unishauri juu ya ubora wa kazi yangu.
 
Samahani kidogo,hebu tuelezee zaidi
MZUNGUMZAJI MHAMASISHAJI ni mtu anaezungumza ktk namna yenye kugusa hisia za msikilizaji na kuweza kumfanya aone anaweza kufanya jambo. Ni ile hali ya kumtoa mtu katika fikra za unyonge na kutojitambua na kumhamishia ktk fikra mpya za kuthubutu na kuweza. Hoja za mzungumzaji hujengwa katika uhalisia na mifano iliyo kweli. Mfano, kampuni inaweza kuwa inapata hasara Lakini hasara ikawa haisababishwi na ama kukosekana kwa mtaji au mazingira ya kazi bali kushuka kwa morali ya wafanyakazi. katika hali kama hii MM anaweza kupewa nafasi ya kuzungumza na wafanyakazi kwa Nia na lengo la kurudisha morali.
 
Au sijakuelewa vzr? Maana hoja yako imejikita ktk wasiwasi ulionao juu yangu na si katika kufahamu kazi zangu. Maana inavyoonekana unataka video ili uone kama kweli mimi ni MZUNGUMZAJI MHAMASISHAJI na si kuona video ili unishauri juu ya ubora wa kazi yangu.

Mimi nilishajua nakuelewa unachomaanisha, lakini kabla sijuita au kuku recomend as a motivational speaker, i must see how good you are...
Una recorded videos za wewe ukifanya yako? Ziweke youtube ili watu wajue unamaanisha nini..
 
Back
Top Bottom