Chief mzuzu
New Member
- Sep 14, 2022
- 1
- 1
*Je, Uchimbaji ni nini?
Ni shughuli inayohusu uchimbuaji wa rasilimali zilizopo chini ya aridhi,nakuziongezea thamani kwa matumizi yakibinadamu.
*Je, Uchimbaji mdogo ni nini?
Maana yake inatafsiri nyingi kulingana na taasisi husika na mtazamo.
Binafsi:Ni mtu au watu wanaochimbua rasilimali chini ya aridhi kwa kutumia teknolojia na vifaa duni kama sokomoko,ponchi,nyundo,koleo nk pasina taarifa za kijiolojia na kijiosayansi kwa kubuni viashiria vya uwepo wa madini.
*Madini yamegawanyika katika makundi matano.
I)Madini ya metali mfano dhahabu,shaba,fedha,nk
II)Madini ya Vito mfano Tanzanite,Rubby.nk
III) Madini ya viwandani mfano jasi,kaolin nk
IV) Madini ya ujenzi mfano kokoto,mchanga.nk
V) Madini ya nishati mfano gas,mkaa wa mawe,uranium nk
*Aina za leseni za biashara ya madini.
Tume ya madini ndiyo yenye mamlaka na dhamana ya kutoa na kusimamia leseni,kukagua migodi na udhibiti wa biashara ya madini.Leseni itoazo.
I) Leseni ya utafiti madini.
II) Leseni ya uchimbaji madini.
a) primary mining license.
b) Mining license.
C) leseni maalum ya uchimbaji.
III) Leseni ya uchenjuaji/uchakataji madini.
IV) Leseni za kununua na kuuza madini.
a)Broker license.
b)Dealer license.
NB: Kila leseni inasheria na taratibu zake
kulingana na kundi la aina ya madini.
*Sera na Sheria ya madini Tanzania.
Serikali ya awamu ya tano,iliyoongozwa na Hayati Dr.John Pombe Magufuli ilifanya maboresho ya sheria ya madini ya mwaka 2010,na kutungwa sheria mpya sura Na. 123 Na.7 ya mwaka 2017 chini ya sera ya madini ya mwaka 2009.Iliyoipelekea Wizara ya madini kujitegemea toka Wizara ya Nishati na Madini.Pia kushirikisha watanzania katika uchumi wa madini na kumtambua mchimbaji mdogo.
Katika historia January 22,2019 Ikulu Dar es salaam Hayati Dr.John Pombe Magufuli alikutana na wachimbaji wadogo, wakati,wakubwa,wafanyabiashara na wadau wakisekta,mkutano uliopelekea maboresho mazingira ya uchimbaji mdogo na biashara ya madini,ikiwa pamoja na kuondolewa baadhi ya tozo na kuanzishwa masoko ya madini nchi nzima.
*Udhibiti na changamoto za kisekta kwa wachimbaji wadogo, wakati na wafanyabiashara ya madini.
Makala hii imejikita kutoa mapendekezo baadhi,ya nini kifanyike kuboresha na kuimarisha mazingira ya uchimbaji na biashara ya madini kwa wachimbaji wadogo na wafanyabiashara katika sekta iliyoajiri watu zaidi ya million 6 za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja (Bina Rais wa FEMATA)
I) Taarifa za kijiolojia na kijiosayansi.
a)Huduma za GST zisogezwe kimkoa ya kimadini kwa gharama nafuu.
b) Taarifa na ramani za kijiolojia na kijiosayansi zipatikane kuanzia ofisi za kata,wilaya,mkoa na kwa maafisa madini wakaazi wa wilaya na mkoa.
c) Wizara ya madini kutenga na kugawa kwa wingi maeneo yaliokwisha fanyiwa utafiti kwa wachimbaji wadogo na kati.
d) GST waanzishe huduma rahisi za awali za kitafiti zinazotembea kuwasaidia wachimbaji machimbo yanapoibuka.
II) Aridhi na Leseni.
a)Tume ya madini ipunguze idadi ya ukomo wa leseni za utafiti toka 20 hadi 5 kwa mara moja,leseni za ziada zitolewe kwa kuonyesha uendelezaji leseni za awali.
b) Leseni zisizoendelezwa pasina sababu maalumu au zakisheria zifutwe wagawiwe wachimbaji wadogo.
c) Sheria ya hakimiliki ya leseni ya utafiti/uchimbaji iboreshwe kwa kumtaka mwombaji afanye makubaliano na mwenye aridhi wajaze fomu na wapige picha katika eneo walilokubaliana,kwa usimamizi wa mkuu wa wilaya.
d) Leseni ya broker isiwe na ukumo wa eneo la kazi.
III) Taasisi za fedha.
a)Stamico ianzishe Stamico bank iatakayotoa mitaji na mikopo,kukodisha na kuuza zana za kazi.
b) Wizara ya madini ianzishe taasisi itakayokuwa mdhamini wa mitaji na mikopo baina ya taasisi za fedha na wachimbaji wadogo,wakati na wafanyabiashara.(kama ilivyo PASS kwa wakulima)
IV)Masoko ya madini na bidhaa zilizongezwa thamani.
a) Stamico ianzishe kitengo cha maduka na masoko kitakacho nunua na kuuza madini ya kimkakati,kuwaunganisha wachimbaji/wafanyabiashara na wanunuzi wa ndani na nje ya Tanzania,itasaidia sekta isiyumbe wakati wa mdororo wa uchumi na wamiripuko ya magonjwa kama uviko-19.nk
b)Miradi ya serikali ifungamanishwe na wazalishaji wa madini ya ujenzi, mfano barabara nk.
c)Ianzishwe mitaa maalumu Tanzania nzima itayokuwa na maduka yakuuza bidhaaa za madini na bidhaa za kiutamaduni.
d)Itungwe sheria itayosimamia shughuli za uongezaji thamani kudhibiti utoroshaji unaofanywa kupitia bidhaa hizo.
V)Elimu,taaluma na ubunifu.
a) Wizara ya madini ianzishe na kuratibu shindano la andiko la mradi kila mwaka,kulea na kuendeleza washindi na kuwaunganisha na wadau,yatakayoibua fikra na fursa mpya.
c) Wizara ya madini kuanzisha jukwaa la mijadala ya uchumi wa madini kwa mwaka mara moja.
d) Wizara ya madini ianzishe mabalozi wa madini.
e)Serikali ibainisha na kuelimisha teknolojia mbadala wa zebaki,na vyuma mbadala wa magogo katika ujenzi wa maduara.
e) Wizara ya madini,wadau wa kisekta na chama cha wanahabari za uchumi wa madini iendesha mafunzo ya kibobevu kwa ajili ya uandaani vipindi,makala nk, vitakavyoelinisha umma.
VI)Ulinzi na usalama kazini na wa rasilimali madini.
a) Msamaha wa kodi kwa vifaa vya usalama kazini (PPE)
b) Wizara ya madini ianzishe kituo cha huduma kwa mteja.
c) vyombo vya Ulinzi na usalama waweke maafisa vipenyo ktk migodi midogo na kati.
d)Ujasusi wa uchumi wa madini na diplomasia ya uchumi wa madini kikanda na kimataifa.
NB:Serikali inatakiwa kufanyia kazi changamoto katika nyanja za,hifadhi ya jamii na bima ya afya,urasimishaji wachimbaji wadogo, mwongozo wa ubia,miundombinu ya barabara,nishati,maji na mawasiliano,afya na mazingira pamoja na teknolojia.
*Hitimisho.
a)Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kuwa na mkutano mkuu mara moja kwa mwaka na wachimbaji wadogo, wakati, wakubwa na wafanyabiashara, pamoja na wadau wakisekta.
b) Wizara ya madini ifungamanishe biashara ya madini na bank kuu ya Tanzania, itasaidia kuimarisha sarafu, kudhibiti mfumuko wa bei na ni dhamana yenye kuaminika isiyo na hatari Duniani.
c) Wizara ya madini kuja na mikakati mipya ya madini hasa yahusuyo mapinduzi ya nne ya viwandani kama Lithium, cobalt, copper, nickel, platinum,3T minerals,REE minerals na madini yatumikayo kutengeneza mbolea,nk.
d) Stamico iboreshwe katika mfumo wa private public partnership na ijisajiri katika soko la hisa Dar es salaam.
Mawasiliano
0629452825.
Chief mzuzu.

Upvote
1