N joo ufanyiwe maombi... Njoo uombewe

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Kila nikirudi home huku napepesuka na kuyumba yumba, na mara nyingine nikiwa sina kumbukumbu viatu nimeacha wapi.
Mke wangu huwa ananipokea kwa upendo na upole sana na kuniimbia huu wimbo wa njoo ufanyiwe maombi, njoo uombewe.
Nlikuwa najua kuwa yeye mama watoto ndio ameutunga kwa sababu sikuwahi kuusikia sehemu nyingine yoyote.
Jana nikiwa mchovu naelekea kilabuni, ndani ya daladala, nikausikia.
Kwa kweli ni wimbo mzuri sana,nyumbani kumsimulia mama watoto kuwa ule wimbo ambao huwa ananiimbia nimeusikia ukipigwa redioni.
Nikakaa na mama watoto wangu nikiwa soba kabisa, dah...
Nikagundua kuwa sasa nampenda wife kuliko nilivyo wahi kumpenda huko siku zilizopita
 
Bonny wa mwaitege.
Wimbo ni mzuri sana na unaburudisha roho na mwili pia
 
Kama unalewa hadi unasahau ulipondondoshea viatu basi ujue kuwa wewe hi hopeless.
Maadamu umegundua unampenda mkeo , nakushauri uwe unarudi mapema na uachane na unywaji wa pombe uliokithiri, ni hatari kwa afya yako.
 

Kanumba style hii.

Yaani unaona unampenda mkeo kwa sababu ya wimbo wa Bony Mwaitege???

Kweli Duniani kuna mambo, bibi yangu aliwahi kuniambia kuwa uyaone!!!
 
jf hiyooo........... yaosha na kusuuza vilivyo..... haya baba wewe fanyiwa hayo maombi uache pombe....ok??na utaacha inshallah 4 the will of allah...😛ray:😛ray::hail:
 
njoo.njoo njoo ufanyiwe maombezi baba wimbo umesimama mnooooo
 
Hongera kwa kurudi kwenye mstari ulio sahihi maana kama ulikuwa unalewa mpaka unasahau viatu si jambo jema na inaelekea kulikuwa na uwezekano wa kuvunjiwa mayai ma..........!!
 
hujawahi kukutana na wale vijana wanaitwa popobawa kwenye harakati zako za miulabu?
 
Na mwisho utauona ufalme wa mbingu. Credit kwa mkeo, badala na yeye kuwa mlevi, kakubadilisha kwa maombi.
 
umenikumbusha mbali Mkuu,
kuna jirani yangu yeye akitoka kirabuni (Mataputapu) usiku mnene anapita na chorus yake moja tu
NInatembea kidogo kidogo nikinyata, basi anairudia hiyo hiyo mpaka anafika home
 
kwa staili hiyo watakupumulia kisogoni !!

ULEVI NOMAAAAA!!
 
Huyu kweli alikuwa ANANYATA maana masanga yakishakubali speed ya kutembea haraka itatoka wapi kama hataki kujikwaa na kuishia mitaroni??!!! POMBE SIO CHAI JAMANI
 
umenikumbusha mbali Mkuu,kuna jirani yangu yeye akitoka kirabuni (Mataputapu) usiku mnene anapita na chorus yake moja tuNInatembea kidogo kidogo nikinyata, basi anairudia hiyo hiyo mpaka anafika home
Duh iyo kali!ananyata nyata!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…