Mfilisiti
JF-Expert Member
- Apr 29, 2020
- 396
- 1,958
Naam ni siku nyingine tulivu na angavu, ili uwe Mwanaume Halisi usiyeyumbishwa kaa hapa fuatana nami hadi mwisho
1: Chochote kile unachokifanya kujitenga na umasikini basi kifanye kwa weledi, Masikini hana dhamana, Masikini haaminiki popote pale, Masikini ni mtu wa malalamiko forever.
2: Kwenye hii Dunia hakuna fedha ya Haramu. Maana fedha hiyo hiyo unayoiita haramu ndio hiyo hiyo inayotolewa madhabahuni na ndio hiyo hiyo inayojenga nyumba nyingi za ibada.
3: Kuna umri ukiufikia jamii huwa haiangalii kile unachofanya, bali jamii huwa inaangalia matokeo tu, na hata jamii ikitokea ikagundua kuwa pesa zako zinapatikana kwa njia isio ya halali bado watakuheshimu tu, na kama ni mtu wa sifa hata machawa utakua nao wa kutosha.
4: Mwanaume, "Pesa, Majumba na Magari ni vitu vya kupita ndio, ila tu hakikisha vinapitia na kwako pia"
5: Mwanaume haitakiwi uoneshe kama umekata tamaa mbele ya watu wanaokutegemea.
6: Ndoa ni taasisi inayotengenza ajira ya kudumu kwa upande wa jinsia ya kike, Hivyo basi hakikisha wewe mwajiri unapotoa ajira hiyo uwe ushafanya feasibility study ikiwa ni pamoja na Cost-benefit Analysis
7: Mwanaume sifa yake kuu ni kuwa provider, Hakikisha unapokua unatoa fedha kwa ajili ya matumizi ya familia yako basi ni vyema hiyo pesa uwe unaitoa mbele ya watoto wako pia wakiwepo, Unapo mpa mkeo fedha chumbani mara nyingi watoto hudhani kuwa mama ndio provider mkuu, ilihali kumbe mama yao ni mwajiriwa mmoja fulani tu kwenye kaya yako hapo.
8: Na ikitokea imethibitika kuwa huo ujauzito ni wako, basi mara moja lea huyo mtoto maana hiyo ni damu yako, ugomvi wako na mwenzio kisiwe chanzo cha mtoto kuteseka na kuyakwepa majukumu.
9: Tambua kuwa unapoleta kiumbe duniani (mtoto)ni wajibu wako kukilinda, na kukihudumia mahitaji yake ya msingi hadi pale atakapo weza kujisimamia mwenyewe.
10: Sio wajibu na lazima kwa mtoto wako kukusaidia eti kwasababu ulimlea, kumusomesha, ili kuepukana na laana uchwara kwa mtoto wako. genye* zako ndio zimemuleta huyo mtoto hivyo kumsomesha ni wajibu.
11: Kama mwanaume hakikisha humbembelezi mwanamke na kufanya vitu vya ziada kama kuhonga ili kumpata, Mwanaume shituka yaani kweli unambembeleza mtu kuja kutumia pesa zako kweli??
12: Mwanaume kumbuka "Usiongeze SMS juu ya SMS isiyojibiwa"
13: Endapo imetokea Mwanaume umeitwa bahiri na jinsia ya kike, basi furahi tena nasema furahi , kwani kwa kufanya hivyo umeweza kukilinda kibunda chako dhidi ya Haramia ambaye hudhania kuwa ana haki ya kupata pesa zako, na wala usijitutumue kuonyesha wewe ni nice guy "so caring"
14: Usijidanganye eti siku moja atakukumbuka kuwa ulikua mtu mwema na kujutia maamuzi yake, pambania kuboresha future yako.
15: Mwanaume, Kopa kiasi unachohitaji, sio kadri unavyoweza kukopesheka.
16: Usitende wema ukategemea utakumbukwa siku ya shida yako. "Always you will be disappointed but make sure you're not surprised"
17: Mwanaume Muda pekee ambao dunia inaamini ni kweli tatizo lako lilikuzidi uwezo ni mpaka pale tatizo ilo likikuua. hivyo jipende, furahia maisha, acha kuchomekea shati lililopauka kwa kigezo cha mtu uliyemwajiri(mwanamke) aishi vizuri.
18: Mwanaume, Ukiona hufukuzii wanawake tena jua umeianza safari yako ya kuingia nchi ya maziwa na asali, hao viumbe huwa wanajileta wenyewe kuna level fulani ukishaifikia.
Mwisho:
Adui unayemmudu usimwachie Mungu.
Mengine ongezeeni wanangu👊
Wassalam