Huu ni uzembe mwingine kati ya 'zembe' nyingi zitokanazo na tume zinazoundwa na rais. Na vile vile ni ushahidi wa jinsi wasomi wa serikali wanavyoshindwa kutoa muongozo wa kutatua kero za wananchi.
Kwa nini hizo tafti hazikushirikisha wanafunzi hata kupitia midahalo ili kupata maoni juu ya utoaji mikopo kupitia vyuo? Mimi naamini wanafunzi wangekuwa na maoni ya msingi kuliko vichwa vya hawa wasomi wa serikali.
Sasa haya yanatokea, bado tuwalaumu wanafunzi wakigoma? Siku za masomo ndo zinaishia, je wakuu wa vyuo wanafanya nini kuzuia hilo? Poleni wanafunzi.
Mkuu nilishaandika siku nyingi kwamba hazina ya serikali imekauka, haina hela za kuwalipa wanafunzi vyuoni. Nikatolea mfano chuo cha SAUT sasa mwezi unaenda kuishi hakuna hata tetesi za boom, wengine wakaponda eti SAUT huwa wanakiherehere cha kufungua mapema. Najua UDSM pressure yenu nikubwa, andamaneni kwani hivi sasa huwezi kudai kitu serikalini mpaka uwape pressure na madhara kutokea.
Mimi ni mmojawapo kati ya watu tunaoteseka kwa hilo. Mpaka sasa nipo home tu, nikiwahi kuja nitakula nini? Nitalala wapi? Bora nijipange, nikawa sawa ndio nije.
tulieni kwanza rais yuko botswana
kwa hyo na wewe huna hata nauli sio?