MAMMAMIA
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 3,811
- 1,607
Wana JF, kauli hii ya mada tayari nimeshaisikia kutoka kwa wavulana wengi ambao wamejibiwa hivi kutoka kwa "marafiki zao wasichana" baada ya kuwataka kwa zaidi ya "urafiki".
Binafsi naamini uwepo wa urafiki baina ya wasichana na wavulana. Kwa kawaida, urafiki wao huwa ni wa kubadilishana mawazo, kupeana moyo, kusaidiana wakati wa shida, hasa pale mmoja anapopata misukosuko katika mahusiano na wachumba zao, na hufanya haya kwa moyo bila kudai fidia.
Katika urafiki huu, mara nyingi mvulana huwa ndiye anayejitolea zaidi. Kwa mfano, ikiwa msichana kaandaa party, mwisho wote wataondoka isipokuwa rafiki mvulana, huyu husaidia kukusanya vyombo na kusafisha nyumba, na ikiwa msichana hana mchumba, rafiki hulala hapo hapo. Lakini mara nyengine, hasa kwa wavulana, hutaka wapige hatua moja mbele, kutoka urafiki kuelekea uhusiano wa kimapenzi na mara nyingi jawabu inakuwa Na mimi ninakupenda pia lakini kama rafiki, na sioni kama kuna ubaya wowote kwa msichana kujibu hivyo.
Swali au wasiwasi wangu kwa nini mvulana hujitolea sana? Ni kwa kutaka kujionesha kuwa yeye ndiye bora na anayefaa zaidi kwa msichana huyo, au hufanya kwa sababu ya urafiki? Ikiwa ni kwa urafiki, kwa nini kutaka kuenda mbele zaidi ya hapo?