Na mvua hizi huu ni muda sahihi wa kununua kiwanja

Na mvua hizi huu ni muda sahihi wa kununua kiwanja

zwangandaba

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2023
Posts
747
Reaction score
1,404
Swalamaa?

Hasa kwa wakazi wa Dar, nyakati hizi za mvua kubwa ndio muda sawia wa kuangalia wapi ununue kiwanja.

Kuna kiwanja nilionyeshwa mwaka jana hapa Dar ila nkatuliza Ili nisubiri kuona msimu wa mvua panakuwaje.

Leo nimekwenda kukagua kabla ya kufanya malipo lakini nilichokikuta nikamshukuru Mungu kwani bado sijatoa fedha kulipia.

Kwa kifupi, nimekuta kiwanja changu tarajiwa wamelima mpunga mpaka na majirani wote hali ni moja

Ukija wakati wa majira yasiyo ya mvua hili eneo liko murua sana
 
Nimenunua Puna Kigamboni!Nimeenda nimekutana na Mashamba ya mpunga,Bora niendelee na ujenzi huku Pugu.
 
Kwa upande wangu, kiwanja ninanunua msimu wowote.

Ukituliza akili, hata kama ni kiangazi unaweza kufahamu eneo hatari.

Iwapo ardhi imenyanyuka na kuna makorongo, basi hapo mafuriko hakuna.

Tatizo watu wengi hupenda viwanja vya tambarare ili kuokoa gharama za ujenzi.
 
Back
Top Bottom