Myujumi Juma
Member
- Oct 31, 2007
- 25
- 0
Mkuu pole sana....au ulisoma hii article kabla ya ajali kukukumba?
Kwanini uangalie in the first place? Hayo ni matatizo ya kujitakia mwenyewe na wala usiwalaumu akina dada wa watu.
Jamani...kwani macho kazi yake nini?
Jamani...kwani macho kazi yake nini? Mbona mnaanza kunilaumu mimi "victim"....? Je ningewabaka hao wadada mngewalaumu wao na jinsi walivyokuwa wamevaa kuwa ndiyo wamejisababishia kubakwa? Kuweni na huruma jamani. Na hii nundu inauma kweli...daaaah
Mkuu pole sana....au ulisoma hii article kabla ya ajali kukukumba?
Mtu unaenda grocery store lakini unavaa kaa unaenda klabu. Umevaa kimini na unaonesha mpasuo/ mgawanyo (cleavage) wa matiti. Matokeo yake mmenifanya nigeuke huku natembea hadi nikajigonga kwenye nguzo ya zege. Sasa hivi nina nundu hapa pembeni ya paji langu la uso kisa mapaja na matiti. Nimechukia sana. Sijui kwa nini mnatufanyia hivyo.....:mad2:
.....uwe unatanguliza ile white stick ati........................
hahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa lol!!!
shem pole jamani, uwe na kiasi na wewe unaangalia tu mpaka mwisho kheee!!!
am trying to imagine hilo linundu usoni kwako duh!!! lakini anagalau umeongeza maisha!!!
Sasa shem na wewe badala ya kunionea huruma unaanza kunicheka. Mambo gani sasa hayo shem....nichemshie maji basi halafu uyaweke kwenye karai halafu unikande kande hii nundu. Sidhani kama Nkwingwa ata-mind wewe kumuuguza shem shem wako....
Wala hatujazidi wewe kwa nini unaangalia mpaka ujigonge upate nundu ya uso??? Unapaswa uangalie kidogo tu kwa sekunde chache halafu uache na wengine waangalie bwana sio wewe unayeangalia mazima mazima
POLE SANA NN...............njoo nikukande bathi hako kathehemu:smile-big:
:hug:
Mtu unaenda grocery store lakini unavaa kaa unaenda klabu. Umevaa kimini na unaonesha mpasuo/ mgawanyo (cleavage) wa matiti. Matokeo yake mmenifanya nigeuke huku natembea hadi nikajigonga kwenye nguzo ya zege. Sasa hivi nina nundu hapa pembeni ya paji langu la uso kisa mapaja na matiti. Nimechukia sana. Sijui kwa nini mnatufanyia hivyo.....:mad2:
Mkuu pole sana....au ulisoma hii article kabla ya ajali kukukumba?
Aaah bana wee...nimetoka zangu kazini nimerudi nyumbani....nikaanza kusumbuliwa na allergies...si unajua huku kwetu tuna matatizo ya pollen. Basi nikaamua kwenda zangu pharmacy pale Kroger kununua Zyrtec. Nikaamua kuangaza angaza kwenye aisles zingine kuangalia kama wana sales zinazoendelea. Ndio humo kwenye aisle nikakumbana na wadada wawili....nadhani wa Wadominican wale....bana weee yaani walivyokuwa wamevaa mtu mzima uzalendo ukanishinda ndugu yako. Waliponipita ikabidi nigeuke tena kuwaangalia huku nikiendelea kutembea. Kichwa kimegeuka nyuma huku naenda mbele. Nikajigonga kwenye nguzo moja ya zile price scanners za kuangalizia bei za vitu. Sasa mwili ulipogonga ile nguzo na kichwa nacho nikageuza na ndipo nikajibamiza pembeni ya paji la uso. Kwenye hiyo aisle walikuwepo jamaa flani wawili na wakaniona nimejigonga...wakaanza kucheka bana. Yaani noma kweli babu......sasa nina nundu halafu wikendi nayo ishafika....sasa hivi hapa nimejiwekea barafu na natumaini uvmbe utakuwa umepungua kufikia asubuhi.....
Mhhhhhh! Kumbe ni dawa...LOL! haya kumbe kazi inayofanywa na macho inaunufaisha mwili mzima maana unakimbiza kabisa BP na heart stroke wala hazikusogelei at the same time increasing your life span hahahahahahah.