Naamini hakuna atakayehoji nia na dhamira ya Hayati Dkt. Magufuli kwa Tanzania,tutaishia kuhoji mkakati aliotumia tu

Naamini hakuna atakayehoji nia na dhamira ya Hayati Dkt. Magufuli kwa Tanzania,tutaishia kuhoji mkakati aliotumia tu

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Nia na dhamira ya JPM dhidi ya Tanzania haitaweza kuhojiwa popote, alidhamiria kutuondoa kwenye umaskini na alitumia mbinu zote kufanikisha lengo. Dhamira iliendana na matendo, Ni vigumu kupata watu kama Hawa Duniani. Watu wanaocha starehe za Dunia nakuwapigania wenzao usiku na mchana. Legacy yako itaishi milele baba. Wasipokuwa wao watakukumbuka watoto na wajukuu zao pale watakapoulizana hivi baba ulifanyia Nini nchi yako?

Hivi babu ulifanyia Nini nchi yako? Kwanini wakati JPM anajiandikia jina usingechapa kazi Kama yeye nasisi tukafahamika? Maswali haya utayajibu ukiwa hai au umekufa. Hao watakaokuwa wanahoji umeifanyia Nini Tanzania wqtakuwa wanapita kwenye reli alizojenga jiwe, maflyover aliyojenga na watakuwa wanasema, kweli mwanaume JPM alifanya Jambo kwa Tanzania.

Kwa Sasa na siku zijazo mtakachoweza kuhoji ni kitu kimoja tu na qmbacho hata Mimi siwakatalii. Mtahoji mikakati yake yakufikia dhamira aliyokuwa nayo. Kuhoji mikakati siyo tatizo maana kila binadamu au taasisi inamikakati yake yakufikia lengo, kinachofanya mikakati iwe mizuri ni lengo lililofikiwa. Kwa JPM hata Kama baadhi ya Mambo aliteleza ila mikakati yake kwa wakati wake imetufumbua macho na kutuvusha kutoka tuliyoamini ayawezekani hadi kuanza kujilinganisha na china na nchi za Ulaya.

Nitaendelea kumtetea mtu yeyote ambaye ana dhamira na nia ya dhati yakufikia lengo, asiyekata tamaa na asiyebebwa na mikakati ya wengine.

Hivyo wakati mnaitupia mawe mikakati ya JPM jiulizeni mikakati yenu imefanikiwa? Kama mmekwama aidha katika ngazi ya familia au taasisi mnayofanyia kazi Basi usisimame kumtupia mawe aliyejaribu na kufanikiwa kwingi huku akifeli kudogo. Tengeneza legacy yako uishindanishe na legacy aliyoacha JPM.

Mimi nilipata nafasi yakuwa mwalimu, naamini wanafunzi wangu popote walipo wanajivunia kuwa na mwalimu Kama Mimi.
 
Naona bado tu unaweweseka. Wenzako baadhi wanajitahidi kuyazoea maisha bila huyo jpm, ila wewe hutaki kabisa kuamini!

Watu wako busy kujadili ripoti ya CAG, wewe uko busy kumpamba marehemu! Hakika kazi unayo.
 
Uliteka na kuua wanafunzi wangapi? Je ulikuwa unaibia watoto wako mtihani ili wafaulu? Huenda hapa tukapata ulinganifu unaotaka kutupatia. Kama ni maendeleo, basi weusi wa Afrika Kusini wanatakiwa wawe wanamsifia kaburi Pieter Botha.
 
Mkuu uko vizuri ila kwenye andiko lako umeyaorozesha mazuri ambayo wengi hatuambiwi tazama yanaonekana ila naomba unifanyie msaada nitajie na yale aliyokosea utakuwa umenifundisha kitu kipya toka kwako na huo ndio uungwana...

Au nakosea ndugu zanguniiiii...?
 
Naona bado tu unaweweseka. Wenzako baadhi wanajitahidi kuyazoea maisha bila huyo jpm, ila wewe hutaki kabisa kuamini!

Watu wako busy kujadili ripoti ya CAG, wewe uko busy kumpamba marehemu! Hakika kazi unayo.
Naona sasa hivi mnacheza mdundiko wa CCM hata Saccos mmeisahau hata Balozi wa Mashoga huko Ubeligji mmemsahau mko busy na Mama Samia.... hahahaha
 
Naona sasa hivi mnacheza mdundiko wa CCM hata Saccos mmeisahau hata Balozi wa Mashoga huko Ubeligji mmemsahau mko busy na Mama Samia.... hahahaha
Kikubwa Tanzania kwanza mkuu, hayo mavyama hayana dili muda huu, tumuunge mkono Samia aunganishe taifa letu Sio Kama yule mwenda zake
 
Back
Top Bottom