Elections 2010 Naamini hatupotei kumchagua Dr Slaa

Mtima

New Member
Joined
Oct 28, 2010
Posts
2
Reaction score
0
Nawashauri wa TZ wenzangu bila kujali itikadi zetu tumpigie kura DR Slaa, kwani kama tumewapa haw ndugu miaka yapata 50 na tumepotea hadi sasa tunakumbwa na lindi la umasikini na ufisadi usioisha, je tukiendelea kuwachagua si ndo tutaendelea kupotea zaidi?

Naamini Dr Slaa ni mtu thabiti tumemuona akiwa na moyo wa kizalendo tangu akiwa Bungeni, akiwatetea wanyonge na kujitoa muhanga kwa ajili ya wa TZ masikini. Mtu huyu anatufaa. Amani itadumu na mshikamano wetu wa TZ uko palepale.

Hata wana CCM msiogope kumchagua Dr Slaa, nadhani hata nyie mnamuelewa, mchagueni tujenge TZ yenye mwelekeo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…