Naamini kuna watu wameweza ku-unlock secret codes za maisha na wanaishi kawaida na sisi kama watu wa kawaida

Ni muda muafaka tuanze kufanya mambo mtambuka sio tu burudani kila muda.

Ahsante mkuu

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Katika kujibu maswali yako, jiulize pia kwanini hivyo vitabu vipo? vilitoka wapi? kwanini vinaaminika sana? kwanini unaishi kwa hofu kuwa kuna Mungu?

So kupata majibu ya maswali yako(ambayo kwa hakika huwezi kuyajibu), tumia kila option juu ya meza, vitabu na hiyo science umesema
 

UKIWA NA MAFANIKIO kila utakalofanya litakua na maana kubwa kwa wasiofanikiwa

Just imagine issue nzito kama hii mtu unatumia lyrics za Chibu au P Square kujengea hoja kwa sababu tu tunawaona wame break the secret code [emoji23][emoji23]
 

Nikijibu haya maswali tutatoka nje ya MADA

Karibu tujadili kuhusu hilo swali lako hapa Uongo mkubwa zaidi kutokea dunia - The biggest scam in the world
 
Kuna ukweli ndani yake... Ukiangalia na kufatilia watu mashuhuri especially wasanii... Kuna vitu wanafanya behind the scenes (kupata fame na success) sidhan kua et kipaj na uwezo binafs ndo viliwatoa. It's all about the secret society.
Mi nimeanza kuhisi kitu kupitia show yao ya full moon party every month kendwa rocks.(Zanzibar)

Ni kua wanajichaj,kufanya rituals kwa wataalamu hapa ndipo pa kuanzia.....
 
Reflection kali kali!
 
Kuna ukweli ndani yake... Ukiangalia na kufatilia watu mashuhuri especially wasanii... Kuna vitu wanafanya behind the scenes (kupata fame na success) sidhan kua et kipaj na uwezo binafs ndo viliwatoa. It's all about the secret society.

Dhana kama hizi ni mbaya sana kwa afya ya ustawi wa maendeleo yako mkuu
Zinafifisha juhudi zako kwasababu unaamini haiwezekani kutoka bila “secret code”

Utajikuta sasa unatumia muda mwingi kwa waganga or whatever kutafuta favor ili utoke badala ya kujibidiisha
 

Mkuu sio udhanivyo... Usifikir mafanikio yanakuja Kwa kuhustle 24/7 nikisema secrete society simaanishi wachawi🤣 hawa ni watu wenyew power duniani ni kama Roma jinsi walivyoteka dini. Sasa kama unafikir kujibidisha ndo mafanikio it's well and good.
 
Sasa wapare wameingiaje hapa 😁
 
Kwa hiyo wa Roma ndio wamempa utajiri Mo Dewji au Bhakresa?

Nyie ndio aina ya watu mnakesha makanisani KUPOKEA utajiri
Au wale kutwa kuhangaika na waganga kusafisha nyota

Mkuu maisha ya kutafuta FAVOR ni utumwa na ujinga.... HAYAPO

Juhudi maana yake sio kukesha masaa 24/7 unafanya kazi...... ni matumizi sahihi ya akili, muda, maarifa na timing

Be very careful mkuu
Kwa akili zako hizi ukichoka umasikini hukawii kumtoa mwanao KAFARA halafu na mali hutapata

Hatuwezi wote kuwa matajiri..... NEVER
Lakini ukiwa na juhudi na akili utaishi maisha yakawaida kabisa na timing ikikubali unatoboa
 
Upo sahihi mkuu, ila Sina mindset ambayo unaniwazia... Nikirejea mada ya Uzi huu, ulikua umebase huko.. ni Hoja tu ndo tumepingana na sio vita. Kwel jitihada na maarifa ndo key to success. Ila Kuna wengine hawavitumii na Bado wako rich. Hili liko Waz kabsa. Ukizungumzia Mo hio ni generational wealth. Bakhresa pia... Hata hivyo Wana consistency ndo maana wealth Yao haishuki. Siamini Uchawi mkuu, ila Kuna watu wananguvu duniani sio za kichawi lakin. Ni kama vile ufalme tuseme.
 
Ndugu,hata mimi naamini kama wewe,jamii za Siri kimekuwa kichaka cha watu fulani kila waonapo mtu kafanya jambo ambalo wao limewashinda au kuwashangaza.
Kuna wazee wa tahajudi,
Kuna wazee wa kukomaa tu na Sheria za ulimwengu,
Kuna wazee wa yoga,
Kuna hawa wataalam wa kutumia dhana/madawa.(wasafisha mwili),
Kuna wengine wako busy na mantras kikamilifu,,,
Kuna wale wanaofanya kazi wanayoipenda wakiwa na furaha sana bila kujali kipato cha kazi hiyo(Hawa huwa matajiri wa jumla(utajiri wao huanzia ndani kabisa)).

Sasa mtu akitoboa kutoka kwenye kundi lolote hapo juu ataambiwa ni SECRET SOCIETY fulani.

Tatizo kingine,akili ya mwanadamu ikishindwa kuelewa jambo fulani linavyofanyika,na akaja mwingine akalifanya kwa usahihi kabisa,,,,basi akili ile itaamini aidha ni MUUJIZA AU UCHAWI ndio uliotumika. Rejea Giza na Nuru.
Ushauri....TUJITAHIDI SANA KUFIKIRI,TUFIKIRI NA TUFIKIRI....NI SIFA YETU KAMA VIUMBE WENYE UTASHI.
 

[emoji419]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…