Naamini mtu anayekufa anajua dhahiri juu ya kifo chake

acontinuer

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2015
Posts
241
Reaction score
246
763fed8c-f938-4ffe-9130-416111548c75.jpg

I believe mtu anayekufa anajua dhahiri juu ya kifo chake, Hivyo kuna uwezekano mkubwa wa kusema kitu fulani kabla ya kifo kumpata.

Undoubtedly true we've seen that several times.

Majira ya saa mbili asubuhi wakati ADAM SHEBA amekwenda kuangalia mwili wa marehemu baba yake

Eneo la mochwari ili kuthibitisha kuwa niyeye au siye.

ADAM alibaini na kuthibitisha kuwa, Mwili ulio ndani ya Jokofu la kuifadhia maiti ni mwili halisi wa baba yake mzazi.

Lakini katika kupepesa kwake macho aligundua

Kuna mende alikuwa anatambaa aneo la uso wa baba yake, hajakaa vizuri akaona mende yule akiishia kwa kuingia kwenye pua ya baba yake.

ADAM akaweweseka kwa mshituko na kupaza sauti "hapana.."

Sauti hii iliwashtua pia walinz wa mochwari na kumuuliza ADAM nini shida

ADAM akasema kuna mende ameingia kwenye tundu la pua la mwili wa baba yake.

Mzee mmoja ambaye ni mlinzi pale mochwari alizungumza kwa dharau "Dogo acha kudata, hujawahi kuona maiti nini..?"

ADAM baada ya kusikia maneno hayo ikabidi azuge kimtindo na ajiweke sawa kisha

Utaratibu wa kutoa mwili mochwari ukaanza kufanyika huku ndugu wakimtaka ADAM akae sehemu na atulie kidogo maana alionekana hayuko sawa..

ADAM alikaa eneo la wazi la hospital ili kupata hewa akiwa na mdogo wake aliyefahamika kwa jina la TIZO..

Wakiwa hapo

ADAM alimuomba mdogo wake akamletee maji ya kunywa ya baridi maana alihisi kiu Isiyo ya kawaida..

Dogo alikwenda haraka kununua maji..

Muda kidogo ukapita, ADAM alikaa hapo

Ghafla ADAM akamuona marehemu baba yake akija eneo alipo huku akiwa na maji ya kunywa mkononi

ADAM akatazama kushoto na kulia aliona watu walio eneo lile la kupumzikia la Hospital wakiwa bize na mambo yao, huku wengine wakipeana habari juu ya hali za wagojwa wao.

ADAM alitazama tena mbele na kumuona Marehemu baba yake akiendelea kuja alipo.

Mara akashikwa bega na alipogeuka alimuona mdogo wake TIZO akimkabidhi maji ya kunywa..

ADAM alipokea maji kwa hofu sana huku akimtazama vizuri mtu anayemkabidhi maji ni mdogo wake au ni yuluyule marehemu baba yake aliyekuwa akimuona..

Alibaini ni mdogo wake kweli..

ADAM alipokea maji na kunywa huku mengine akijimwagia kichwani mwake..

kwakuwa maji yale yalikuwa ya baridi yalimpa utulivu kidogo.

Hapo ndipo ADAM na TIZO wanapewa taarifa kuwa

taratibu za kuchukua mwili zimeshakamilika.

Hivyo watapaswa kuusafirisha mwili huo mpaka kijijinj kwao ambako ndiko watapokwenda kufanya maziko ya baba yao..

Bila kupoteza muda, gari ikaja na mwili ukaingizwa na sasa ni safari ya kwenda huko kijijini ikaanza

Wakiwa njiani ADAM

Akawaza namna alivyomuona mdudu yule kule mochwari akiutambaa mwili wa baba yake, na akawaza namna baba yake alivyomtokea akimletea maji ya kunywa..

Akajiuliza mwenyewe hiyo ina maana gani..? However hakupata majibu yoyote..

Akiwa katika mawazo hayo ADAM akapitiwa na usingizi.

Mara akaota yupo kwenye chumba kikubwa chenye kiza sana.

Ndani ya chumba hicho kunaonekana kuwa na mwili mmoja wa maiti, maiti hiyo ilizungumza kwa sauti kubwa ikisema ADAM usiniache"..

Ajabu sauti hiyo ilikuwa

ni ya marehemu baba yake..

ADAM aliogopa na kutaka kutoka kwenye chumba hicho lakini hakukuwa na mlango ndani ya chumba hicho.

ADAM akawa anaangaika na mwisho akashituka yupo ndani ya gari Huku mdogo wake TIZO akimuuliza nini shida mbona anatoka jasho isiyo ya kawaida.

ADAM hakujibu chochote badala yake aliomba maji ya kunywa.

Waliendelea na safari.

Afterwards walifika kijijini kwao usiku sana

Vilio vya akina mama vilitawala kijijini pale.

Huku vijana wa kiume wakishirikiana kuushusha mwili wa Marehemu kutoka kwenye gari na kuuingiza ndani.

ndugu wengine wakatelemka huku ADAM naye akifuatia kutelemka..

Wakati ADAM anatelemka kwenye Gari alikutana na

Mzee mmoja wa pale kijijini anayemfahamu na kumuheshimu.

Mzee akamvuta pembeni ADAM wakasalimiana huku mzee akimpa pole.

Kisha mzee huyo akamwambia ADAM kuwa amemuona akiweweseka juu ya kifo cha baba yake.

Mzee akasema hiyo ni ishara ya kifo tata.

Mzee akamtaka ADAM

aende sambamba na mwili wa marehemu mpaka kwenye chumba utakachohifadhiwa kabla ya maziko.

Mzee akamsisitiza ADAM atakapofika chumbani hapo asitoke bali anapaswa kuwa kwenye chumba hicho hili kuulinda mwili wa baba yake.

Pia akamsihi asiruhusu watu ambao si watoto wa marehemu

wakakaa wenyewe kwenye chumba cha marehemu🤔

Mzee akamaliza kuwa amebaini baba wa ADAM hakufa kwa kifo cha kawaidia..

Na Ili kuthibitisha hilo, wakati ADAM atakapokuwa kwenye chumba cha marehemu kuna mtu atakuja na kuomba abaki mwenyewe kwenye chumba cha marehemu

Huyo ndiye mtu anayehusika na kifo cha baba yao.

ADAM hakubishana na maneno ya mzee, na kwakuwa yeye ndiye mkubwa kuzaliwa, akawadokeza wadogo zake juu ya ujumbe huo..

Wadogo zake wakamtaka yeye ndiye aende huko chumbani kuulinda mwili wa baba yao..

ADAM akakubali bila

Kujiuliza mara mbili.

Akiwa chumbani pembeni ya mwili wa marehemu baba yake, alishudia ndugu ambao ni watu wazima wakiingia na kumpa pole.

Majira ya saa tisa usiku akaja

Mama mzazi wa ADAM..

ADAM baada ya kumuona mama alinyanyuka kwa heshima na kumkumbatia huku machozi yakiwatoka kwa pamoja.

Kila mmoja alikuwa na huzuni, ADAM akihuzunika kumpoteza baba, huku mama akihuzunika kumpoteza Mume...

Wakazungumza kwa muda kisha mama akamuomba ADAM

Ampishe anataka kubaki mwenyewe ili azungumze maneno ya mwisho na marehemu mumewe

ADAM baada ya kusikia maneno hayo ya mama akakumbuka alichoambiwa na yule mzee🤔

Je kama wewe ni ADAM utatoka chumbani au utabaki?

Itaendelea.
 
View attachment 3056081

Mambo ya hadithi nusunusu hatutaki hapa.

Andika hadithi yako ikikamilika copy ndio uje kuipaste hapa.
 
Back
Top Bottom