Naangamia mwenzenu nisaidieni pls!

Gambaz

Member
Joined
Oct 9, 2011
Posts
75
Reaction score
2
Mi ni kijana wa kiume natafuta sana kazi maisha magum huku mtaani. Nina digrii ya UHASIBU pia ujuzi wa computer eg MS word,excel,power point,database na email and internet. Nafaham pia computerized accounting packages such quick book,equinox and Tally. Nina uzoefu wa mwaka mmoja. Nipo tayari kufanya kazi popote na yeyote ile. Asanteni sana.
 
mkuu,nakushauri ujiajiri,kuna wafanyabiashara wengi siku hizi wanataka kufanya outsource ya huduma za uhasibu,trust me,utafanikiwa sana,ni dili ya maana,fanya utafiti kwa watu wanaofanya huduma hizo upange gharama zako halafu weka contacts zako hapa tukutafute,usiwe common scholar ambae anatafuta ajira,ajira cku hizi sio what u know bali ni who u know,follow my advice,u have somethin to sell,ur profession,jiuze.
 
Hii wazo la kuajiriwa sijui lini litafutika akilini mwetu! Una degree ya uhasibu! kwanini usijiajiri? ungeomba wana-JF wakupe Ushauri wa namna ya kujiajiri ningekuona wa maana sana!
 
mwanaCBE nina point 3.6,.don kamanga nashukuru sana kwa ushaur wako,nimekuPM kwa maelezo zaidi. Mchakamchaka tatizo ni Capital ndg yangu...
 
Tembelea ofisi za FINCA-Tanzania, head office ni maeneo ya Manzese huwa wanachukua watu kimyakimya: na wenye fani kama yako ndo wanachukuliwa kwa sana pale: Confidence juu ya kile unachokijua ni muhimu popote uendako hata kama una vyeti vizuri.
 

Ndugu yangu pole. Kinachokuangamiza ni mawazo yako tu ndugu, kwanza ujifunze kuona umuhimu wako na value yako, maneno kama naangamia, maisha magumu inatosha kuona ila nikushauri wewe ni bora zaidi ndugu, kazi utapata, pia anagalia mazingira yako, utajiajirije, sio lazima kuajiriwa, kinachotumbuaga wala sio capital ni jinsi tunavyoangalia mazingira, you are the best kaka! Kila la kheri ndugu yangu
 
Gambaz,biashara za kutoa huduma capital sio ishu,kwa ishu ya ofisi unaweza kuanza nyumbani unapokaa,hata chumbani kwako.
 
tembelea ofisi za finca-tanzania, head office ni maeneo ya manzese huwa wanachukua watu kimyakimya: Na wenye fani kama yako ndo wanachukuliwa kwa sana pale: Confidence juu ya kile unachokijua ni muhimu popote uendako hata kama una vyeti vizuri.
magomeni mwembe chai
 
Fikiria kujiajiri sio kuajiriwa kwani hata ukipata hiyo kazi sana sana utalipwa laki 3 sasa itakupeleka wapi bado hujatoa nauli, kuonga kale kademu kako, chakula, nyumbani na n.k , jamaa 1 amealiza pale CBE kitambo tu anafanya ishu zake binafsi tena started with zero capital lakini leo hii amefanya makubwa na anatumia elimu yake Kufanya biashara Sio kuwa na mawazo mgando ya kutaka kuajiriwa. Imagine Bill gate today angekuwa na mawazo kama yako kipindi hicho leo angekuwaje!!!!!
 
Jamani kujiajiri issue mitaala yetu haina ata chembe ya elimu ya ujasiriamari.
Mwana tafuta ata kamtaji kadogo tuu ujianzie mdogo mdogo serikali haina habari na job creation na hata sijui iyo wizara ipo pale inafanya nini?
Pole one day Yes never loose hope.Unaweza drop CV na vyeti vyako pale CRDB Azikiwe huwa wanachukua wahasibu!
 
Ukishindwa kabisa jichakachue, msomi kama wew unashindwa kuanzisha vi2 vya kukuungizia income je hao ndugu zako ambao hawajasoma!!!
 

hivi unaanzaje na hiyo zero capital, natamani sana kujiajiri.
 
Una degree,wkt upo chuo hilo bumu la laki 7 na 20 ulilitumbua lote??? Hapo ndio mnakosea kazi za kuajiriwa siku hizi ni ngumu,ilibidi uwe unasave incase ukiwa mtaani uweze kufanya mambo nakushauri fungua hata genge hili usukume siku yl unatafuta kazi.
 

we unaongelea bumu? Kama huna point si bora ukae kimya...una uhakika gani kama alikuwa na bumu ..je unayajua mazingira aliyokuwa nayo?
 

Pole mwanangu.
Ninakushauri uandike barua kwa ufupi tu ya kuomba kazi. Tengeneza CV yako safi kabisa na usisahau kuweka referees wakuaminika watatu. Ambatanisha na vyeti vyako (IV, VI na chuo). Jitahidi upate address za mabenki yafuatayo: CRDB, NMB, NBC, AKIBA COMMERCIAL BANK, STANBIC, STANDARD CHARTERED BANK, EXIM.
Hakikisha unapeleka barua, CV na vyeti kwa mabenki yote haya. Kisha potezea kabisa na uendelee na shughuli nyingine. Utashitukia unaitwa kwenye Interview hata kama ni baada ya mwaka mmoja. Hakikisha unaweka contacts zako ambazo hazina utata haswa simu. Mara nyingi hawatumi barua, bali wanakupigia simu ya mkononi. Hizi Bank hawatangazi nafasi za kazi hata siku moja. Wanaita wale walioomba ambao tayari wana docs zao nilizotaja hapo juu.
Binti zangu wawili wamepata kazi CRDB kwa mtindo huu. Infact CRDB walikuwa na Interview ya watu almost 300 wiki mbili zilizopita na wameajiriwa wengi tu bila upendeleo hata chembe, including mabinti zangu. Nasikia Interview nyingine itakuwa mwezi wa saba. Nakutakia kila la heri na Mungu akutangulie mwanangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…