Naanza kuwaelewa kataa ndoa! Mama Ayubu amuua mumewe kisa anarudi nyumbani bila pesa yoyote!

Naanza kuwaelewa kataa ndoa! Mama Ayubu amuua mumewe kisa anarudi nyumbani bila pesa yoyote!

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Mwanamke anayefahamika kwa jina la Mama Ayubu mkazi wa mtaa wa Banda mbili Kata ya Sombetini Jijini Arusha, anadaiwa amemuua mume wake aitwae Daudi Estomii (45) ikiwa ni baada ya kuwepo kwa tuhuma za muda mrefu kuwa amekuwa akimpiga mwanaume huyo pindi anaporejea nyumbani nyakati za usiku huku akiwa hana chochote mkononi mwake.

Inaelezwa kuwa mbali na tukio hilo mwanamke huyo siku za hivi karibuni alifanya jaribio la kutaka kumnyonga mama mkwe wake kwa mtandio kutokana na kitendo cha mama huyo kutaka kuingilia kati ugomvi wa mwanae na mwali huyo.

Aidha, Inaelezwa kuwa licha ya mwanaume huyo kushushiwa kipigo mara kwa mara, hakutaka mke wake achukuliwe hatua zozote za kisheria kwa madai kuwa hawezi kumshtaki mke wake kwenye vyombo vya sheria.

Kadhalika, baada ya kuwepo kwa madai hayo wananchi wenye hasira kali wamevamia na kuvunja nyumba ya marehemu kwa madai kuwa mwanamke huyo pamoja na wanae wawili hawatakiwi kuishi katika nyumba hiyo kwasasa kwakua wote kwa pamoja wanadaiwa kuhusika na mauaji hayo.

 
R.i.P Classmate...😥
Pamoja na kumshauri sana, lakini alikomaa kuoa bondia...😕
Kataa ndoa.....
Ndoa ni mauaji..😪
 
Screenshot_20250214-213835~2.jpg
 
marehemu ndicho alikitaka, maana akiambiwa mke wake ashtakiwe hataki aya kamuacha mamake anahangaika huku
 
kifo cha daud estomii kutokana na kipigo toka kwa mkewe hakiwezi kuharamisha ndoa.
 
Inabidi sasa kuwe na chama cha kutetea haki za wanaume especially wanaopigwa na wake zao tuwe na dawati letu la jinsia .

Na muache kuoa mabondia
 
Back
Top Bottom