Naanza upya na biashara ya Nafaka rejareja, nipeni Muongozo

Naanza upya na biashara ya Nafaka rejareja, nipeni Muongozo

Vinci Dayot Upamecano

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2020
Posts
524
Reaction score
1,288
Ishini sana, Tabu sio jambo jema lakini hatuna budi kuzipitia.

Kuna kibanda nimekiotea kipo soko la mtaani, hilo soko halina watu wengi saana ila pilika pilika zipo kimtindo pamoja na makazi ya watu sio uswahilini sana sio ushuani sana ni changanyikeni flani hiv nataka niweke kambi hapo...

Nimeuza bajaj niliyokuwa nakorogea, sikupenda ni baada ya songombingo flani kunivagaa nimejikuta naisukuma kwa Bei ya hasara (Tsh4,470,000/) ila nimebakiwa na kama 1M na points kama mtaji.

1. Sina uzoefu ndiyo naanza kazi
2. Sina mishe nyingine pembeni nitategemea hapo
3. Bado sijajua nijikite zaidi na nafaka gani, mawazo yangu; (Mchele, Maharage, Mahindi ya makande, Mbaazi, Kunde, Mafuta ya Alizeti na Karanga labda na Dagaa wa mwanza)
4. Bado sijajua napata wapi hizo nafaka
5. Changamoto zake + hasara
6. Mbinu za kuepuka point no.5
7. Faida zake zikoje [emoji4][emoji39][emoji847]
8. Mengineyo...

Semeni chochote nipate kupona

(Wabilah toufeeq)

Silog off Y
 
Kama unataka kufanikiwa na hio biashara usiifanye tegemezi, tafuta kitega uchumi kingine otherwise utapoteza mtaji wako wote.
 
huku kwetu NJOMBE MAKETE Kuna wingi wa viazi vp hiyo kitu huwez fanya??
Pia Kuna mkaa mwingi
Debe 5 viaz 45,000/
Gunia mkaa 10,000/
Ukichukua vingi ndo Bei inapungua
Mm sio muuzaji wa chochote hapo just an idea
 
Akichukua anauzia wapi
 
Akichukua anauzia wapi
hapo alipo sema amepata fremu au aangalie sehemu nyngne pia Ili asifanye biashara Moja ndo tegemezi ikianguka anaanza upya Tena ni Bora akawa na hata 2 au 3 Ili Moja iwe life support nyngne dream support
 
Mtaji wake si umeuona lakini,?1 m
 
huku kwetu NJOMBE MAKETE Kuna wingi wa viazi vp hiyo kitu huwez fanya??
Pia Kuna mkaa mwingi
Debe 5 viaz 45,000/
Gunia mkaa 10,000/
Ukichukua vingi ndo Bei inapungua
Mm sio muuzaji wa chochote hapo just an idea
Wazo zuri sanaa hilo broo robbertisaah uminiongezea idea Mchele unaenda sambamba na viazi... Lakini mkuu naskia biashara ya mkaa saiv wanatakatisha sanaa!
 
Mtaji wake si umeuona lakini,?1 m
Ndio mkuu nmeuona ndo maan nikatoa kama wazo ye apime pia kipi kinaweza kikampa turn over ya haraka na uhakika au hata ushauri wangu akautumia baada ya kuanza hiyo biashara ya nafaka coz nlichokiona hapo n kwamba atafeli maan kuanza biashara Moja then ndo ikupe Kila hitaji lako na ijiendeshe ni ngumu kama ana ndoto za kukua kibiashara ila inawezekana kama atakua anafanya biashara Ili aendlee ku survive mjini tu
 
Wazo zuri sanaa hilo broo robbertisaah uminiongezea idea Mchele unaenda sambamba na viazi... Lakini mkuu naskia biashara ya mkaa saiv wanatakatisha sanaa!
Kuna Uzi nlipitia kuhusu maswala ya mkaa na nahis Kuna mahali upo humu TAFUTA utapata.
Jamaa alizungumza kwamba mwanzon wakat wa kuanza biashara ya mkaa itakutoka pesa ndio lakn vibali vitakua vya mwaka ndo vitacost Hela nyng ila the rest utakua unalipa ushur mdogo wa kawaida Kwa Kila gunia so kuanziaa hapo utakua huru na utapata faida coz ukishakua huru hauuzi Kwa kujificha ndpo hata watej utawapat wengi
Ila ukifanya kiwizi utapata wateja Wachache wanaopafahamu hapo unapouzia hao tu na sio wateja wapya so hiyo itafanya uone kama hakuna faida mkuu
 
Kama unataka kufanikiwa na hio biashara usiifanye tegemezi, tafuta kitega uchumi kingine otherwise utapoteza mtaji wako wote.
Chief Amante nina kauwezo kadogo cha kushona viatu vip wakati nikiwa nasubiria wateja siwezi kushona-shona viatu kupata hela ya kidogo ya mboga? Au ntakuwa bored kwa wateja, labda waneza kuniona sipo serious!!!?
 
Back
Top Bottom