Naanza upya na biashara ya Nafaka rejareja, nipeni Muongozo

Daaah unazidi kunifungua Asante sana, maana hii biashara nimeidhamiria kweli.
 
Chief Amante nina kauwezo kadogo cha kushona viatu vip wakati nikiwa nasubiria wateja siwezi kushona-shona viatu kupata hela ya kidogo ya mboga? Au ntakuwa bored kwa wateja, labda waneza kuniona sipo serious!!!?
Hiyo pia Iko poa mkuu coz utaifanya Kwa nje ya ofisi Yako pale mlangon inakua ni kama biashara inayojitegemea ila inaweza kua bored Kwa wateja coz unaweza ukawa na wateja wa 2 wa viatu wanasubir huduma then wakaja wateja wa nafaka wa 2 na Wana maelezo maréeeeefu huon kama wa nje wataona hauko siriaz
 
Hiyo bajaji ndipo hela ilikuwapo, umebugi sana kuiuza. Au ulikuwa unakaa foleni vijiweni bila kujiongeza.

Maana kwenye bajaji ukiwa unajituma kwa siku hukosi 15,000 hadi 20,000. Ila vijiweni humu hautapata mafanikio kwa haraka utachoma muda wako na faida haitaonekana.

Huku kwenye biashara ya nafaka inataka mtaji mkubwa sana ili uweze kuifanya kama biashara. Ukiwa na mtaji chini ya million 5 utakuwa unafanya baishara ya kusukuma siku na sio biashara serious ya kupata faida na kukuza mtaji na kuendesha maisha yako.

Mazao ya nafasaka yana mambo kama misimu ya mavuno ambayo ili kucheza nayo inabidi uwe nakiasi kizuri cha pesa kama mtaji ili uweze kumudu kununua stock kulingana na uhitaji wa soko lako.

Sasa dah kwasababu ulishauza bajaji yetu sijui tunafanyaje hapo.
 
@Samcezar dooh moja haikai, mbili haisimami... Hiv mazao ninunue kwa wale mawakala wa sokoni, au niingie tu bush alone?
 
Nakushauri chukua bidhaa moja tuu kwanza mfano mchele, kama kuna uwezekano kuchukulia chaka kabisa sio kwa hawa wa mjini huko utapata Kwa bei nzuri sana. Nimekushauri uchukue bidhaa moja kwanza Kwa sababu
-mtaji ni mdogo na ni vyema wakati unaanza ubaki na pesa kidogo ku push biashara yako.
-itakuwia rahisi kupata mzigo mwingi Kwa bei nzuri.

Baada ya hapo cheza na bei, hakikisha unamfanya mteja aje kwako kwa kutumia mbinu ya bei, uza Kwa bei fulani hivi ambapo utawauzia watu wa rejareja lkn hata watu wa jumla wangetamani kununua kwako, namaanisha pata faida ya 100 lakini mzigo uende haraka.

Ukikomaa unaweza kuongeza bidhaa zingine taratibu.
 
Nashukuru sana kwa ushauri wako Lothbrok
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…